Na Mwandishi wetu, Babati
KADA
maarufu wa Mjini Babati Mkoani Manyara, Emmanuel Khambay, amechukua
fomu ya kuomba kupitishwa kugombea nafasi ya mjumbe wa Mkutano mkuu wa
CCM Taifa kupitia Wilaya ya Babati Mjini.
Khambay
amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa CCM wa Wilaya ya Babati Mjini
Daniel Muhina, ambapo atagombea nafasi moja kati ya tatu zitakazogombewa
ya mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Taifa kupitia Wilaya ya Babati.
Khambay
ambaye ni kada maarufu mjini Babati na Manyara kwa ujumla kutokana na
kushiriki kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo, amethibitisha
kuchukua fomu hiyo ila hakuwa tayari kuzungumza na vyombo vya habari kwa
sasa.
Kwa upande wake,
Katibu wa Jumuiya ya UVCCM Wilaya ya Babati Mjini, Idd Sulle amechukua
fomu ya kuomba kugombea nafasi ya Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa
CCM mkoa wa Manyara.
Kada
maarufu wa CCM mjini Babati, Cosmas Bura Masauda amejitosa na kuchukua
fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Babati Mjini.
Naye,
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la COSITA, Patrice Gwasima,
amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Babati
Mjini.
Wanachama na
makada mbalimbali wa CCM wapo kwenye mchakato wa kuchukua fomu za
kugombea nafasi mbalimbali ambapo hatua ya matawi imeshafanyika na
kuendelea ngazi ya Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...