Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndg Abdulrahman Omar Kinana amewataka viongozi na watendaji wa serikali kuhakikisha wanarahisisha ufanyaji wa shughuli za wananchi kwa kuwaondolea vikwazo kwa kuwa sekta binafsi inaanza na wao.
Kinana ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jimbo la Nkasi Kaskazini eneo la Lyazumbi wakati wa mapokezi ya kuanza ziara mkoani Rukwa akitokea mkoa wa Katavi.
"Serikali inafanya jitihada za kuimarisha na kuboresha mazingira ya sekta binafsi nchini ili ifanye vizuri, sasa sekta binafsi inaanza na wananchi wa kawaida. Tuwaondolee kero wananchi wetu na tuwarahisishie kufanya shughuli zao iwe ni wakulima, wafugaji, bodaboda, wamachinga au wafanyabishara." Amesema Kinana
Akimkaribisha mkoani Rukwa Mwenyekiti wa CCM mkoa huo Ndugu Rainer Lukalah
amemueleza Ndg Kinana kuwa hali ya siasa katika mkoa huo ni shwari na wanaridhishwa na kazi kubwa ya maendeleo inayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Kinana ameingia mkoani Rukwa ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya uimarishaji chama na ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...