Mafundi sanifu wa maabara za kupima Ubora wa Bidhaa zitokanazo na Mimea dawa kutoka Taasisi mbalimbali nchini wametakiwa kushirikiana katika kazi zao ili kuhakikisha bidhaa hizo zinazozalishwa nchini ziweze kufikia soko la kimataifa na kuchangia katika pato la watengenezaji na taifa.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Shahada za Juu, Utafiti uhawilishaji wa teknolojia na ushauri wa kitaalamu Prof. Esron Karimuribo wakati akifunga mafunzo ya siku nne matumizi ya vifaa vya kiasasa vya upimaji ubora kutoka katika taasisi mbalimbali za Serikali nchini ambazo zinahusika katika kuchunguza ubora.
“Sisi sote ni Watanzania tunajenga Taifa moja hatushindani sisi kwa sisi hivyo ni wajibu wetu kushirikiana katika kazi zetu ili kusaidia kufanikisha jukumu tulilopewa la kusimamia ubora na hasa pale inapotokea changamoto kwa mmoja wenu muwe tayari kusaidiana ili kazi zifanyike kwa ufanisi” alifafanua Prof. Karimuribo.
Kwa upande wake Kiongozi wa mafunzo hayo kutoka Chuo Kikuu cha corpenhagen nchini Denmark Prof. Bjarne Styrishave amesema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa GRILI na Shirika la Misaada la maendelo la Denmark DANIDA ambayo kwa pamja yanasisitiza umuhimu wa uchunguzi wa viwango vya kemikali kwenye mimea dawa ili kulinda afya ya watumiaji.
“Ili malengo hayo yatimie lazima Tanzania iwe na wataalamu wengi na wenye uwezo wa kutumia vifaa vya kisasa vya uchunguzi maana teknolojia zikakua kila siku lakini pia mafundi hao wawe na uwezo wa kuvifanyia matengenezo madogomadogo pale vinapopata hitilafu badala ya kuvitupa au kuhitaji kupelekwa nje ya nchi kwa matengenezo hivyo mafunzo haya sasa yamewapa uwezo huo na kupitia ushirikiano wataweza kufanya kazi zao vizuri” alibainisha Prof. Bjarne.
Amesema kwenye mafunzo hayo ameona mchanganyiko wa wataalamu kutoka Taasisi mbalimbali nchini inagwa inawezekana wengine hawafanyi kazi za kupima ubora wa bidhaa za mimea dawa lakini jambo kubwa na la msingi wanafanya kazi za kufanya uchunguzi wa ubora wa vitu mbalimbali na kifaa cha kisasa zaidi duniani ni LC/MS ambacho kimefundishwa na kipo SUA.
Amesema kupitia DANIDA wameweza kukamilisha maabara nzuri na kuweka vifaa vya kisasa kama vile LC/MS/MS vya upimaji ubora na viambata katika mimea dawa lakini mafunzo hay ani sehemu ya kuhakikisha endelevu wa uwezo na uchunguzi wa ubora wa baidhaa mbalimbali nchini maana mradi ni wa miaka mitano lakini shughuli hizo zinatakiwa kue ndelea hata pale mradi utakapomalizika.
“Mradi umesaidia kusomesha wanafunzi sita wa Shahada ya Uzamivu na wanafunzi wawili wa shada za Uzamili nab ado tunaendelea kuona na namna zipi tunaweza kuzitumia kuahakikisha kazi hii inaendelea baada ya mradi kuisha na mkakati wetu wa kwanza ni ushirikiano ndio maana tumewaita Mafundi sanifu hawa kutoka taasisi mbalimbali nchini wanaofanya kazi hizi wafahamiane na kujenga ushirikiano” aifafanua Dkt. Mabiki.
Awali akieleza malengo ya Mafunzo katika mradi huo Mkuu wa Mradi wa GRILI Dkt. Faith Mabiki amesema mafunzo hayo yanalenga katika lengo la msingi la kwanza la mradi huo la kuhakikisha wanajengea uwezo wataalamu katika kwenye kwenye maswala ya matumizi ya vifaa na uwezo wa kupima ubora na kemikali za mimea dawa.
Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo kutoka Chuo cha Ufundi Arusha Bwana Meshack Timoth na Mkuu wa Maabara ya upiamaji Ubora wa Udongo,Maji na mimea ameshukuru kupata nafasi ya kushiriki mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwa vitendo zaidi katika kutumia kifaa hicho cha kisasa kilichopo SUA.
“Pamoja na kujifunza lakini mafunzo yametupatia nafasi ya kufahamiana na kushrikiana miongoni mwetu kutoka taasisi mbalimbali na hii itatusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinapotokea miongoni mwetu” Alieleza Fundi sanifu huyo wa maabara bwana Timoth.
Nae Mshiriki kutoka Mamlaka ya maabara ya mkeimia Mkuu wa Serikali bwana Edward Dilunga amesema mafunzo hayo yamewasaidia kuwaongezea ujuzi katika utekelezaji wa majukumu yao hasa ikizingatiwa kuwa sayansi inakua na teknolojia mpya zinazalishwa kila siku hivyo mafunzo hayo yataongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.
“Kwangu mimi binafsi kama Mkemia imeniongezea ujuzi zaidi ya ule niliokuwa nao katika uchakataji wa Sampuli kwa kutumia kifaa hiki cha kisasa cha LC/MS HP/LC ambavyo vyote hivi ni vifaa ambavyo kwenye Ofisi ya Mkemia mkuu wa Serikali vipo lakini ni faida kwa taasisi yangu maana elimu niliyoipata itasaidia kuboresha utendaji wangu na kuleta matokeo chanya katika ofisi yangu,” alieleza Bwana Dilunga.
Kwa upande wake Afisa mthibiti Ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Tatu Yusufu amesema mafunzo yamemsaidia kuongeza uwezo kwenye kutumia HPLC mashine ambayo wameanza kuitumia kwa sasa kwenye maabara yao na GC ambayo anaitumia hivyo mafunzo yamekuwa na msingi mno katika kazi zao.
“Sisi TBS hatutumii HPLC /MS na TC kwahiyo hapa nimeongezewa ujuzi mpya wa kuchanganya mashine hizo zote kwa pamoja kwenye matumizi na hivyo nimeona kuwa HPLC/MS kwa pampja inafanya vizuri zaidi kuliko ukizitengenisha”Alifafanua BI.Tatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...