WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata ya Nanganga wilayani Ruangwa.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Julai 4, 2022) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa kata hiyo akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika kata hiyo ikiwemo ya afya, elimu na maji.

“Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa umwagiliji Nanganga, tutumie vizuri bonde letu. Vijana changamkieni fursa hii kwa kuanzisha kilimo cha mbogamboga na mazao mengine.”

Mheshimiwa Majaliwa ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa uendelee na mpango wa ujenzi wa soko la mboga mboga katika Kata ya Nanganga ili kuwawezesha wakulima wa mazao hayo kupata sehemu ya uhakika ya kufanyia biashara.

Amesema Serikali imetoa shilingi milioni 447 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa usambazaji maji Nanganga na shilingi milioni 31 kwa ajili ya kusambaza maji katika kijiji cha Mbecha na shilingi milioni 470 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Mchenganyumba.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka wanafunzi wajitahidi kusoma kwa bidii kwa sababu mbali na Serikali kutoa Elimsingi Bila Ada pia imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu mbalimbali ya kutolea elimu nchini.

Mheshimiwa Majaliwa amekagua mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Nangumbu, zahanati ya kijiji cha Mtakuja pia, ametembelea shule ya msingi Ndandawale pamoja na kuwasamia wananchi wa kijiji cha Chimbila na kuwasisitiza waendelee kufanya kazi kwa bidii Serikali ipo pamoja nao.

Awali, Diwani wa Kata ya Nanganga, Bw. Kambona aliishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika kata hiyo ikiwemo miradi ya maji ambayo imeweza kutatua changamoto ya uapatikanaji maji.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua maji katika eneo maalum la kuchotea maji katika Shule ya Msingi Mbecha wilayani Ruangwa kabla ya kuwasalimia wananchi, akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi , Julai 4, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi katika viwanja vya Shule ya Msingi, Mbecha wilayani Ruangwa akiwa katika ziara ya Jimbo lake la uchaguzi, Julai 4, 2022. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Teleck. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...