Na John Walter-Babat
MBUNGE wa Jimbo la Babati Vijijini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Daniel Sillo amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ameonesha kwa vitendo azma yake ya kuinyanyua sekta ya kilimo na wakulima ili izidi kutoa ajira kwa Watanzania wengi zaidi.
"Kwa mara ya kwanza tumeshuhudia kwenye Nchi
yetu hii ni bajeti ya kwanza inaletwa na Serikali na hakuna mtu
analalamika kwamba ni ndogo hapa nimpe pongezi Rais Samia kwa hakika
ameonesha kuwajali watanzania kwa vitendo, maslahi ya wakulima,wafugaji
na wavuvi"alisema.
Amesema bajeti hiyo italeta mapinduzi makubwa
kwenye sekta mbalimbali hivyo kupanua wigo kwa walipa kodi na kuongeza
malighafi za viwandani.
"Niipongeze Serikali kwa kuongeza bajeti ya
Kilimo hadi kufikia Sh Bilioni 751,kundi kubwa la vijana linakwenda
kushiriki Kilimo" alisema Sillo.
Aidha amewaambia wakazi wa Jimbo la
Babati Vijijini kuwa bajeti hiyo itagusa sekta ya afya ambapo vituo vya
afya vya Madunga,Bashnet na Ayasanda na Gidas vitakwenda kukamilika
pamoja na Zahanati ambazo hazijakamilika.
Serikali imewasilisha
bungeni bajeti yake kuu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo jumla ya
shilingi trilioni 41.48 zinatarajiwa kutumika. Shilingi trilioni 28.02,
zitatokana na vyanzo vya ndani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...