Na Mashaka Mhando, Muheza

MBUNGE wa jimbo la Muheza Hamis Mwinjuma maarufu MwanaFA, ametoa baiskeli 200 kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kutoka katika kata 37 zilizopo katika jimbo hilo, ili kuwapunguzia mzigo wa kutembea umbali mrefu kwenda shuleni.

Akikabidhi baiskeli hizo za kisasa kabisa, mbunge huyo alisema amekabidhi baiskeli kwa wanafunzi 200 ambao kigezo kilichotumika kuwapata ni wale  wanaoishi mbali na shule wanazosoma ili ziwasaidie kupunguza changamoto ya umbali wa kwenda na kurudi kutoka shuleni.

MwanaFA alisema baiskeli hizo ni msaada kutoka kwa marafiki zake wa taasisi ya Kimarekani ya Wheel 2 Afria ambayo wamemuahidi kumsaidia baiskeli nyingine atakazozigawa katika awamu ya pili, kukabiliana na tatizo la umbali kwa wanafunzi.

"Hili kwangu lilikuwa  Personal (binafsi) kwavile niliyaishi maisha haya ya kutembea umbali mrefu kupambania elimu na najua watoto hawa walivyokuwa wanajisikia wanavyokumbana na hii changamoto ya umbali," alisema mbunge huyo.

Alisema anaishukuru taasisi ya Kimarekani ya Wheel 2 Afria kwa kumuwezesha kuwasaidia watoto hao jambo ambalo linakwenda sambamba na kumunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuondoa ada kwa watoto wa kidato cha sita katika bajeti ya mwaka huu.

Akizungumza wakati akikabidhi baiskeli hizo, Katibu wa CCM mkoa wa Tanga Suleiman Mzee Suleimani alipongeza juhudi za mbunge za kuwarahisishia maisha wanafunzi hao na akasisitiza kwamba jambo hilo CCM inajivunia kupata mbunge mwenye maono yanayotatua changamoto kwa wananchi.

"Hiki unaweza kuona ni suala dogo lakini hapana, maono uliyotumia kuja na wazo hili la kuwasaidia watoto hawa baiskeli ni jambo linalopaswa kuungwa mkono na wana Muheza no jambo kubwa, umefanya," alisema Katibu huyo na kuwataka wananchi wa jimbo hilo kumuunga mkono mbunge wao kwani ni mbunge makini, "Muheza mmepata mbunge anayejali matatizo yenu," 






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...