Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
WAPENZI wa masumbwi nchini leo Julai mosi wanatarajia kushuhudia mpambano mkali baina ya mabondia, Mfaume Mfaume na Abdumonem Said kutoka nchini Misri.
Pambano hilo la ngumi za kulipwa la kuwania mkanda wa Ubingwa wa WBF uzito wa kilo 79 raundi 10 linafanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Upanga, jijini Dar es Salaam likiwa limeandaliwa na kampuni ya Grobox .
Akizungumza wakati wa kupima uzito bondia, Mfaume amewataka watanzania kuwa na imani naye na wategemee ushindi katika pambano hilo kutokana na mazoezi aliyoyafanya chini ya Kocha wake Ramadhani Jah.
“Kipindi nilipokuwa kambini nimefanya mazoezi kama mnyama ili kujiweka fiti zaidi na kuwapa burudani na ushindi Kwa nchi yangu ."
Kwa upande wake bondia Abdumonem amesema atahakikisha anafanya vizuri katika pambano hilo kurejea na ushindi nchini Misri.
“Nimekuja Tanzania kwa lengo la kushinda, nimefurahi nimepata mapokezi mazuri ila ushindi lazima nipate."
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...