Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
BONDIA wa Ngumi za kulipwa nchini Mfaume Mfaume ameshinda mkanda wa ubingwa wa Afrika (WBF) baada ya kushinda KO raundi ya pili dhidi ya mpinzani wake kutoka Misri Abdulmonen Said katika pambano la "Return of Naccoz king"
Aidha bingwa huyo amesema alijiandaa vizuri aliweka kambi miezi mitatu Mkoani Morogoro Kwa ajili ya kupambania mkanda huo na kuiletea ushindi nchi ya Tanzania.
Hata hivyo Mfaume amesema ana tambua uwezo wa mpinzani wake kwani Kwa nchi ya Misri ni Bondia mzuri na ameshacheza mapambano 22 na yote amefanya vizuri huku pambano Moja akitoa sare na mpinzani wake.
Pia amesema ushindi huo ni Kwa Mashabiki zake na watanzania wote Kwa ujumla wanaopenda mchezo wa Masumbwi.
"Huu ubingwa ni watanzania wote nimeweza kubakisha mkanda nyumbani nashukuru Kwa wote waliohakikisha mkanda huu unakuwa wa watanzania".
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...