Na. Damian Kunambi, Njombe
Kutokana na madhara mbalimbali ambayo yamekuwa yakijitokeza katika kusafisha mashamba kwa kuchoma moto , wakulima kote nchini wametakiwa kuacha tabia ya kusafisha mashamba kwa njia hiyo pasipo kibali maalum na endapo watabainika kufanya hivyo watahukumiwa kwenda jela kwa miaka isiyopongua 15 bila faini yoyote.
Akizungumza hayo wilayani Ludewa mkoani Njombe Mtaalamu wa kufuatilia moto wa misituni hapa nchini Kekilia Kabalimu mbele ya waziri wa maliasili na utalii Balozi Dkt. Pindi chana, viongozi wa TFS, mkuu wa wilaya na viongozi wengine ngazi ya wilaya katika mafunzo ya uhifadhi misitu na vipimo amesema kifungo hicho ni kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai sura ya 16 kifungu cha 321 na 322.
Amesema Kuchoma moto misitu au mashamba kunahitajika kuomba kibali kwenye kamati ya maliasili ya kijiji akiwa na watu wasiopungua watano ambao atashirikiana nao katika zoezi hilo la uwashaji moto.
"Ukisha patiwa kibali unatakiwa uwe na wasaidizi watano watakao andikisha majina yao na atayarishe barabara yakukinga moto yenye ukubwa kulingana na urefu wa nyasi za shamba lake". Amesema Bi. Kabalimu.
Aidha kwa upande wa mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere amesema zaidi ya asilimia 75 ya maeneo wilayani kwake yameathiriwa na moto kwa kipindi cha mwaka jana wakati wa uandaji mashamba hivyo ametoa onyo kujirudia kwa jambo hilo katika kipindi cha mwaka huu bali watunze masalia kwaajili ya mbolea.
Amesema mashamba yaliyo mengi yanakosa rutuba ya kutosha kutokana na kuharibiwa na moto kitu ambacho wangeweza kutunza masalia ya shambani ambapo yatakapooza yanakuwa mbolea asilia.
Naye waziri wa Maliasili na utalii Balozi Dkt. Pindi Chana amesema atakapofanya ziara kwa wakati mwingine wilayani hapo atapita katika mahakama kuona idadi ya kesi zilizo wasilishwa juu ya uchomaji moto pasipo vibali.
"Moto unaathiri sana shighuli za maendeleo ya nchi, unakuta kuna mtu kila mwaka ni lazima awashe moto na kuathiri mashamba ya miti na mali za watu hivyo watakao bainika wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria". Amesema Balozi Dkt. Pindi Chana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...