Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
BAADA ya kumaliza mkataba wa awali wa miaka mitano, Klabu ya Simba imeandika barua ya kufika kikomo cha kutoendelea na mkataba mpya na Kampuni ya Sportpesa, mkataba wa awali ulidumu kwa kipindi cha miaka mitano tangu May, 2017 uliposainiwa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Nwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Sportpesa, Abbas Tarimba amesema Kampuni hiyo ilipokea barua ya kutoendelea mkataba mwingine baada ya kufika kikomo cha mkataba wa awali.
“Jana tumepokea barua kutoka Simba SC ikitufahamisha kwamba, mkataba wetu na wao wa kipindi cha miaka mitano kuanzia May, 2017 umefika tamati”, amesema Tarimba.
Amesema Sportpesa wamepokea taarifa hiyo, na kuwatakia kila la kheri kwenye udhamini na Kampuni nyingine.
“Tungependa kuendelea nao lakini lazima tuheshimu maamuzi ya kila mmoja, sisi tunajivua kwenye miaka mitano ya kupata mafanikio makubwa ya kunyanyua viwango vya timu ya Simba SC”, ameeleza
Amesema, Sportpesa imefurahi kumaliza mkataba huo bila misuguano au migogoro yoyote na Simba SC, amesema Sportpesa wataendelea kuwepo kwenye Soka sanjari na kudhamini timu nyingine mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...