Na Karama Kenyunko Michuzi TV

Mkazi wa Chamanzi, Abdul Abdallah (35) na mkewe ,Salma Mshamu (21) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu ikiweno kukutwa na nyara za serikali ikiwemo meno 413 ya Tembo  yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 4.04  na meno mawili ya Kiboko yenye thamani ya Sh milioni 3,453,000.
 
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa Serikali Mwandamizi Timotheo Mmari imedai washtakiwa pia na shtaka la kujihusisha na biashara ya nyara za serikali.

Imedaiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Pamela Mazengo kuwa kati ya Januari Mosi, 2017 hadi Septemba 3, 2019 maeneo ya Saku Chamanzi wilaya ya Temeke Mkoani Dat es Salaam washtakiwa walinunua na kupokea meno 413 ya Tembo yenye thamani ya USD 1,755,000 Sawa na sh 4.040,010,000 pamoja na meno mawili ya mnyama, Kiboko yenye thamani ya USD 1500 Sawa na sh 3,453,000.

Katika shtaka la pili ikadaiwa kuwa washtakiwa kwa pamoja walikutwa na meno 413 ya Tembo yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 4.04 mali ya serikali ya Tanzania bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mkurugenzi wa wanyamapori.

Washtakiwa pia wanadaiwa kukutwa na meno mawili ya Kiboko yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 3.4 mali ya Tanzania bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mkurugenzi wa wanyamapori.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi umeishakamilika na sasa wanasubili kibali kutoka kwa mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) aweze kuridhia kama shauri hilo liendelee mahakamani hapo.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo kwa kuwa ni la uhujumu uchumi na baada ya uchunguzi kukamilika litapelekwa katika Mahakama ya Mafisadi.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 2,2022 kwa ajili ya kutajwa


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...