Wananchi na kijiji cha chakama kata ya Matawale jimboni  la Masasi mjini Mkoani Mtwara julay 01.2022 wameanza kupata huduma ya Maji safi na salama kwenye kijiji chao Kama ni Moja ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeeleo kupitia chama Cha Mapinduzi ( Ccm).

Huu ni muendelezo wa jitihada za  Serikali ya JAmhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia suluhu Hassan ambayo imejipanga kutatua kero za Wananchi wake kwa kushirikiana na  Mheshimiwa Mbunge Geoffrey Mwambe na Ruwasa Masasi Ili  kuhakikisha wananchi na wakaazi wa maeneo yote ya Masasi  ikiwemo maeneo ya pembozoni mwa mji wananufaika na huduma hii ya Maji safi na salama.

Katika kuhakikisha Wananchi wanapata huduma ya Maji kwa uhakika  kwenye kijiji hiki cha chakama vitajengwa vioski takribani vitano vya kutolea Maji na Tanki kubwa lenye ujazo wa lita elfu hamsini(50000LT) tayari limeshajengwa kijijini hapo.

Upatikanaji wa huduma ya Maji safi na salama kwenye kijiji cha chakama Kwa miaka mitano iliyopita yaani 2015/2020 ulikuwa ni 0% kwani hapakuwa na mradi wowote badala yake wananchi walikuwa wakitumia vyanzo vya asili ambavyo sio salama kwa matumizi kama vile mito, na mabwawa Hali amabayo ilikuwa inahatarisha Afya za Wananchi hao.

Kwa upande wao Wananchi wa Kijiji hicho wametoa pongezi kwa Serikali ya JAmhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia suluhu Hassan kwa kuwajali na kuonyesha upendo wa dhati Katika kutatua Changamoto mbalimbali za kijamii ambazo ni kero Kubwa zilizokuwa zinawakabili kwa muda Mrefu.

 Baadhi ya wanawake waliopo Katika Kijiji hicho Wanatoashukrani kwa Serikali ya Mama Samia suluhu Hassan kwa kuwatua Ndoo kichwa I kwani wamepitia Changamoto kubwa sana kipindi Cha ambacho Huduma ya Maji haipatikani Katika eneo lao ,ikiwemo Ndoa zao kuharibika kwa sababu wanawake hao walikuwa wanatumia muda mwingi kwenda kutafuta maji  mabwawani.

"Tulikuwa tunaamka mapema kwenda kutafuta Maji mabwani huko na tukifika huko tunakuta foleni hivyo inakubidi ukae  usubirie Ili urudi na Maji nyumbani kutokana na foleni basi Kama umeenda saa 12 asubuhi unarudi saa nane mchana hapo hujapika bado Sasa mwanaume akikuona anajua kule ulikuwa umekaa tuu au unafanya vitu ambavyo havieleweki basi Ugomvi unaanza na hata Taraka unapewa"

"Lakini Sasa hivi kwakweli tunamshukuru Rais Samia suluhu na Mbunge wetu Kwa kutatua kero hii maji na tunamuahidi basi tutaendelea kuonyesha Ushirikiano na Serikali yetu Kwani inawajali Wananchi  wake wa chini Kama Wananchi wa hapa Chakama "wanasema Wananchi.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...