Na Janeth Raphael

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Bwana Raymond Mndolwa, leo tarehe 6 Julai, 2022 amesema, mwelekeo wa Sekta ya Umwagiliaji katika kipindi cha miaka mitatu yaani 2022 - 2025 ni kuongeza eneo linalomwagiliwa kutoka hekta 694,070 za sasa hadi hekta 1,200,000.

 Raymond Mndolwa ameyasema hayo, mbele ya Wanahabari katika ofisi za Tume ya Umwagiliaji, Kikuyu, Jijini Dodoma.

Mndolwa amesema ili kuhakikisha lengo linafikiwa; Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji itaendelea kuboresha miundombinu ya umwagiliaji iliyoharibika na isiyofanya kazi, pamoja na kukamilisha ujenzi wa miundombinu katika skimu mpya.

"Tutafanya upembuzi yakinufu na usanifu wa kina ili kujenga skimu na mabwawa mapya ya kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya shughuli za kilimo cha umwagiliaji". Amesema Mndolwa.

Mndolwa amesema, Tume ya Umwagiliaji inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Dira ya Taifa ya Maendeleo Awamu ya Pili, Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II), Mpango wa Umwagiliaji wa mwaka 2018 na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020.

Aidha; Mndolwa amesema, Wizara ya Kilimo kupitia maelekezo ya Mheshimiwa, Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imewawezesha Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa kuongeza bajeti kwa zaidi ya asilimia 600.
Mndolwa amemshukuru, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Umwagiliaji pamoja na kibali cha ajira ya Wataalam 344.

“Tunamshukuru, Rais wa Awamu ya Sita kwa kibali cha kuajiri, idadi kubwa ya Wataalam kwenye Taaisi yetu pamoja na hilo namshukuru Waziri wa Kilimo kwa uteuzi wa timu nzuri ya Wajumbe wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji”.

"Tume imepewa majukumu ya kuratibu, kuendeleza na kusimamia maendeleo ya Sekta ya Umwagiliaji nchini, Tume ilianza rasmi kutekeleza majukumu yake tarehe 15 Septemba, 2015 na ninamuahidi, Mheshimiwa Rais kuwa, nitatekeleza majukumu yangu kwa ufanisi mkubwa." Amesema  Mndolwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...