Na Shamimu Nyaki – WUSM

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Saidi Yakubu ameridhishwa na kasi inayoendelea ya ujenzi wa  Jengo la kudumu la wizara hiyo.

Akizungumza alipotembelea eneo la ujenzi Julai 19, 2022 Mji wa Serikali  Dodoma, Bw. Yakubu amempongeza Mkandarasi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kuongeza kasi pamoja na Idadi ya wafanyakazi ambao umechagiza hatua ya kuridhisha katika ujenzi

“Leo kazi inaonekana, mmepiga hatua, nimeona idadi ya wafanyakazi imeongezeka, vifaa vya ujenzi vipo vya kutosha pamoja na malighafi nyingine”alisema Bw.Yakubu.

Aidha, amesisitiza Mkandarasi huyo kuongeza usalama maeneo ambayo yanachangamoto ili watu wasijekuumia, pamoja na kuhakikisha eneo la kupanda miti pamoja na maua linaonekana haraka iwezekanavyo ili miti na maua yapandwe kama alivyoelekeza Waziri wa  Mkuu wa Tanzania  Mhe. Kassim Majaliwa.

Kwa upande wake Mkandarasi wa Jengo hilo Ahmad Abdalah amesema amepokea maelekezo yote na pongezi alizotoa Naibu Katibu Mkuu, ambapo ameahidi kukamilisha ujenzi huo mwezi Oktoba 2023.

Jengo hilo  lenye ghorofa sita kwa sasa limefikia asilimia 30 ya ujenzi na linatarajiwa kuwa na kumbi za mikutano ya ndani, sehemu za michezo na matanki ya maji yenye  ujazo wa lita milioni nne pamoja na eneo la kupumzikia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...