Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) inashiriki Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia yenye kauli mbiu "Elimu ya Juu inayokidhi Mahitaji ya soko la ajira kwa maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi" yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini(TCU) ili kuonesha huduma mbalimbali zinazotolewa na Bodi hiyo pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi waliofika kwenye Banda la Bodi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Idara ya Elimu na Mafunzo wa NBAA, Peter Lyimo amesema huduma zinazotolewa na NBAA katika kipindi cha maonesho ya Elimu ni Usajili wa Wanafunzi ili kuweza kufanya mitihani ya Bodi hiyo kwa ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya chini (Accounting Technician) mpaka ile ya Taaluma (Profession) pamoja na usajili wa wanachama na makampuni ya kihasibu na Kikaguzi.

Pia Lyimo amesema NBAA wanatoa huduma zote ikiwemo jinsi ya kujisajili kufanya Mitihani, malipo ya Ada kwa Wanataaluma, ametoa wito kwa wote wanaotaka kufanya usajili kwenye Bodi ya NBAA wale wanaotaka kusajiliwa kufanya mitihani ya Bodi wanatakiwa kufika katika Banda lao lililopo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

"Bodi hiyo kwa sasa mfumo wa kidijitari wa kutoa huduma zake hususan usajili wa wanafunzi na Wananchama kupitia tovuti yao, amesema huduma hizo zinapatikana hata ukiwa sehemu mbalimbali pia kwa sasa huduma hizo zimehamia Mnazi Mmoja.

Amesema mwaka huu wa 2022 Bodi ya NBAA inatimiza miaka 50 toka kuanzishwa kwake mwaka 1972 hivyo ni jambo la kujivunia kwa kuweza kusimamia taaluma ya Uhasibu hapa nchini pamoja na maadili yao kwenye sehemu zao za kazi.
Meneja wa Idara ya Elimu na Mafunzo wa NBAA, Peter Lyimo akiwa kwenye picha ya pamoja na Wafanyakazi wenzake wa NBAA katika Banda la Bodi hiyo kwenye Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia , yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini(TCU) yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa NBAA, Sawa Ngendabanka( wa pili kushoto) akitoa maelezo kuhu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo kwa mwananchi waotembelea banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) kwenye Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia, yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini(TCU) yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Wafayakazi kutoka Bodi ya NBAA, Deodatus Soka(wa kwanza kulia), Hassan Kawambwa pamoja na Salim Kasumariwakisiliza maswali yaliyokuwa yanaulizwa na mwananchi aliyetembelea banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) kwenye Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia , yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini(TCU) yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Mfanyakazi wa Bodi ya NBAA, Salim Kasumari akijibu maswali pamoja na kutoa elimu kwa mwananchi aliyetembelea banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) kwenye Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia , yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini(TCU) yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Mfayakazi kutoka Bodi ya NBAA, Deodatus Soka(wa kwanza kulia)akitoa maelezo kwa mwananchi kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo aliyetembelea banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) kwenye Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia , yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini(TCU) yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Katikati ni Salim Kasumari kutoka NBAA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na wakuu wa Taasisi mbalimba baada ya kufungua Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Julai 19, 2022.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...