Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango akimkabidhi Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja  wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Yesaya Mwakifulefule  kikombe cha mshindi wa kwanza katika kundi la bima walioshiriki Maonesho Biashara Kimataifa Sabasaba yaliyohitimishwa leo Julai 13, 2022 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Yesaya Mwakifulefule akionesha kikombe cha mshindi wa kwanza katika kundi la Bima  walioshiriki Maonesho Biashara Kimataifa Sabasaba yaliyohitimishwa leo Julai 13, 2022 jijini Dar es Salaam.

 Wafanyakazi wa NIC wakifurahia ushindi kikombe  cha ushindi wa kwanza katika kundi la bima walioshiriki Maonesho Biashara Kimataifa Sabasaba yaliyohitimishwa leo Julai 13, 2022 jijini Dar es Salaam.

 

SHIRIKA la Taifa la Bima (NIC) limeibuka mshindi katika  kundi la kampuni za Bima zilizoshiriki katika maonesho  ya 46 ya Biashara Kimataifa Sabasaba yaliyohitimishwa Julai 13, 2022.


NIC imepokea kombe la  ushindi huo kutoka kwa Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango.


Akizungumza mara baada ya kupokea  ushindi huo Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja Yesaya Mwakifulefule amesema ushindi huo ni kwa shirika kutokana na kutoa huduma bora kwa wananchi wakati maonesho hayo.

Mwakifulefule amesema kuwa licha ya kuibuka mshindi kwa mara ya pili mfululizo baada ya mwaka jana, kazi yao kubwa ni kuendelea kuwa bora katika kutoa huduma za bima nchini.

Aidha amesema kuwa katika kuonyesha ubora wa huduma kwa wananchi na wadau wa bima kazi kubwa ni kuongeza bidhaa za bima kutokana na mahitaji yaliyopo.

Mkurugenzi huyo amesema wafanyakazi wasibweteke kwa ushindi huo bali kuuendeleza kila panakuwa na ushindani ambao utatokana na kunyesha uwezo wetu katika kutoa huduma za Bima nchini.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...