Kocha mpya wa Timu ya Polisi Tanzania kutoka nchini Burundi Joslin Sharif Bipfubusa (Katikati) akisaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja. Kulia ni Katibu Mkuu wa timu hiyo ASP Michael Mtebene na kushoto ni Mwanasheria wa timu hiyo Joram Mwakansope. Hafla hiyo ilifanyika Makao Makuu ya Polisi Dodoma. (Picha na Timu ya Polisi Tanzania)
Mwenyekiti wa timu ya Polisi Tanzania, Kamishna wa Polisi Charles Mkumbo (Katikati) akizungumza wakati wa kumtambulisha Kocha mpya wa Timu ya Polisi Tanzania kutoka nchini Burundi Joslin Sharif Bipfubusa (Kushoto) Hafla ya utambulisho ilifanyika Makao Makuu ya Polisi Dodoma. Kulia ni Katibu wa timu hiyo ASP Michael Mtebene (Picha na Timu ya Polisi Tanzania)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...