Bodi ya Wakurugenzi ya PSPTB chini ya mwenyekiti wake Jacob Kibona leo tarehe 21 Mwezi 08, 2022 imeidhinisha  na kutangaza matokeo ya mitihani ya 24 katika ngazi mbalimbali za masomo ya Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).

Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB), Godfred Mbanyi amesema mitihani hiyo ilifanyika mwezi Mei hivyo kupitia Bodi hiyo anatangaza rasmi matokeo ya mitihani ya 24.

Mbanyi amesema watahiniwa waliokuwa wamejiandikisha kwa ajili ya kufanya mitihani hiyo walikuwa ni 1031 lakini walioweza kufanya mitihani walikuwa ni 971 na kati ya hawaliofanya mitihani watahiniwa 458 sawa na asilimia 47.2 wamefaulu mitihani yao, watahiniwa 457 sawa na asilimia 47.1 wamefaulu baadhi ya Masomo na watahiniwa 56 wao wamefeli kabisa na watatakiwa kurudia kurudia mitihani yao kwa ujumla.

"Watahiniwa wote wanaweza kumtazama matokeo yao kupitia tovuti ya Bodi ambayo www.psptb.go.tz  na pia matokeo hayo yatatumwa kwenye akaunti ya kila mtahiniwa ili kurahisiha upatikanaji wa tokeo yao" alisema Mbanyi.

Pia amesema wale wote wenye mitihani ya marudia wanatakiwa kijiandaa vizuri kwa mtihihani yao ya mwezi wa 11 ili waweze kufahulu vizuri.

"Tathmini inaonesha kwamba katika mitihani hii ya 24 kuna baadhi ya Masomo yamefanyika vizuri na watu wamefaulu vizuri na Masomo hayo yalikuwa sita lakini kuna Masomo machache hasa yale ambayo yanahusisha hesabu kumekuwa na changamoto Sana kwa watahiniwa wa Bodi kutokufanya vizuri Masomo hayo" alisema Mbanyi

Amesisitiza kuwa wale wote wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi wanatakiwa kuwa wanahudhuria kwenye vituo vya kujiandaa na mitihani maana changamoto ni kuwa vijana wanajiamini kupita maelezo na kuvibeza vituo hivyo na kupelekea kufanya mitihani ya Bodi bila kuhudhuria vituo ambavyo vimesajiliwa na Bodi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB), Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa anatangaza matokeo ya mitihani ya Bodi ya 24 yaliyoidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi wa PSPTB makao makuu ya Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...