Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Salum Masoud Attai,alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Soko la Samaki Malindi linalojengwa na kampuni kutoka Japan,wakati akiendelea katika ziara yake ya Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali
Mwinyi alipokuwa kizungumza na wananchi mara baada ya kutembelea ujenzi
wa Hospitali ya Mkoa inayojengwa katika Shehia ya Lumumba Wilaya ya
Mjini akiwa katika ziara yake ya Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini
Magharibi.[Picha na Ikulu] 18/07/2022.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Bibi.Bimkuwa Nassor (kulia) mwakilishi wa kikundi cha wakulima wa Mwani “SUBIRA NZURI” mara baada ya kukabidhi vifaa vya Uvuvi pamoja na boti za kupakilia mwani akiwa katika ziara ya Wilaya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi na wananchi wakiwa katika hafla ya kukabidhi vifaa vya Uvuvi pamoja na boti za kupakilia mwani viliyokabidhiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwa katika ziara ya Wilaya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Fedha Shilingi Millioni Moja na Nusu Nd,Kassim Hassan akiwa mshindi katika mashindano ya Vidau wakati ziara yake ya Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.[Picha na Ikulu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa araza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wavuvi, wakulima wa mwani pamoja na Wananchi mara baada ya kukabidhi vifaa vya Uvuvi akiwa katika ziara ya Wilaya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...