Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKUU
wa mkoa wa Pwani,Abubakar Kunenge amewataka wananchi wa kata ya
Mbwawa kutafuta eneo jengine la kujenga kituo cha Afya kutokana na eneo
la Kwanza kutokidhi vigezo na masharti ya Serikali .
Aidha ametoa maelekezo kuwa kituo cha Afya cha awali kifanyiwe marekebisho kwa kujenga wodi ya wazazi.
Kunenge
pia ameagiza wananchi hao kutumia fedha walizouza trekta Shillingi
milion 9 kuanza ujenzi wa wodi ya wazazi katika zahanati hiyo.
Agizo
hilo amelitoa, wakati wa mkutano wa wananchi wa kata hiyo baada ya
kutokea mgogoro wa ardhi katika eneo la ujenzi wa kituo hicho.
Kunenge
amewaeleza wakazi wa Mbwawa kuwa, eneo walilolichagua ambalo lina
ukubwa wa hekari 6 ni ndogo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha
Afya, na kwa mujibu wa katiba ya nchi kituo cha Afya kinatakiwa kuwa
na hekari 15.
"Utaratibu
wa kujenga kituo cha Afya ni lazima eneo liwe na ukubwa wa hekari 15
"sasa eneo hili no hekari 6 tu hivyo halitoshi badala yake nataka eneo
hili mjenge wodi ya wazazi" alisema Kunenge.
Amewaeleza, wananchi wa Mbwawa kutumia eneo hilo kwaajili ya ujenzi wa wodi ya
wazazi na amewaruhusu kutumia fedha hizo Shilingi milioni tisa kuanza
ujenzi wa wodi ya wazazi na kusema serikali ya Mkoa kupitia Halmashauri
itasaidia kumalizia ujenzi huo.
Awali
akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mkuu wa Wilaya ya Pwani Bi. Sara Msafiri
alimueleza Mkuu wa mkoa kuwa eneo hilo la Mbwawa linahitaji kuwa na
kituo cha Afya Kwani ni eneo lenye wananchi wengi na wanapata
changamoto ya kufuata huduma za Afya katika kituo cha Mlandizi
Sara
alieleza kuwa walishafanya utaratibu wa kutafuta eneo lingine la
kujenga kituo cha Afya, badala ya eneo la awali kutokukidhi vigezo.
Aliendelea
kusema tayari serikari ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mama
Samia imeshatoa Shilingi Bilioni 2 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha
Afya Cha kisasa kwani eneo hilo lina watu wengi na wanahitaji huduma ya
afya.
Sara pia
alifafanua kuhusu sintofahamu iliyojitokeza kuwa eneo la awali lenye
ukubwa was hekari 6 Lina mgogoro na kusema kuwa eneo hilo ni Mali
halali ya serikari na halina mgogoro wowote.
Aliendelea
kusema Kama Kuna mtu anadai eneo ni lake basi aende Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa na nyaraka sahihi na taratibu za kisheria zitafatwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...