Na Said Mwishehe, Michuzi TV
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala ametoa rai kwa wakazi wa mkoa huo na Watanzania kwa ujumla kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika mapambano ya vita dhidi ya dawa za kulevya nchini.
Aidha ametoa ushauri kwa Ofisa Elimu Mkoa pamoja na wadau wengine zikiwemo mamlaka zinazoongoza mapamdano ya vita dhidi ya dawa za kulevya kuangalia kama inawezekana machapisho yanayotoa elimu inayoelezea madhara yake yanaweza kusambazwa shule za sekondari ili wanafunzi wafahamu mapema madhara yatonakayo na utumiaji wa dawa hizo.
Makala ameyasema hay oleo Julai 1,2022 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja mkoani Dar es Salaam alipokuwa akifungua kilele cha Maadhimisho ya Kupinga Matumizi ya Dawa za Kulevya ambayo kitaika yamefanyika katika mkoa huo.
Akizungumza zaidi Makala aliyekuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa maadhimisho hayo amesema Dar es Salaam ni miongoni mwa mkoa ulioathirika na dawa za kulevya, hivyo wananchi wa mkoa huo na mikoa jirani na Taifa kwa jumla kushirikiana dawa za kulevya.
“Mapambano dhidi ya dawa za kulevya hayatamalizwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya peke yake bali inahitaji ushiriki wa kila mmoja wetu, tukishiriki kikamilifu tutafanikiwa.
“Wakati napita kwenye mabanda yaliyoko kwenye viwanja hivi nimewasilikiza wadau kuhusu ushiriki wao kwenye mapambano haya na kila mmoja ana umuhimu wake.Hata hivyo nimeona na machapisho na nimeyachukua, yanaelezea madhara ya dawa za kulevya.
“Na nimeambiwa kesho(Julai 2)kutakuwa na uzinduzi wa kitabu kinachozunguzia madhara ya dawa za kulevya lakini kuna machapisho mengi yaliyochapishwa na wadau na naamini yakisambazwa yatakuwa msaasda mkubwa katia kuelimisha umma.
“Nimeomba iwapo itawezekana machapisho yawe yanakwenda kwenye shule za sekondari ili yakatumike kutoa elimu kwa wanafunzi .Athari za dawa za kulevya ni kubwa na kuna hatua mbalimbali zinaendelea kukomesha dawa hizo na wale wenye uraibu wanaendelea na matibabu ya kupewa dawa za Methadoni,”amesema Makala.
Amesisitiza umuhimu wa wananchi hasa wazazi na walezi kufuatilia nyendo za watoto wao ili kuhakikisha hawajiingizi kwenye matumizi ya dawa hizo.“Mtoto anapoingia kwenye utumiaji dawa za kulevya kila ambacho anakiangalia yake kwake ni biashara, anauza chochote ili apate anachotaka,
“Hivyo jamii ni muhimu sana kuangalia watoto wetu, ndugu zetu ili kuwaokoa, leo tuko kwenye mapambana ya panya road lakini wengi wao ukiwauliza wanakwambia kabla ya kuingia kwenye kufanya matukio wanavuta bangi ili waweze kushika mapanga na kujeruhi.Bangi ni sehemu ya dawa za kulevya, “
Aidha amesema Mamlaka ya Kudhibi na Kupamba na Dawa za Kulevya wakiongozwa na Kamishina Generali Gerald Kusaya wamekuwa wakifanya kazi kubwa kukomesha dawa za kulevya na hata wale wachache wanaofanya biashara ya dawa hizo wanaona Tanzania sio salama wao kuendelea na biashara hiyo.
Ameomba ombi kwa mamlaka nyingine ikiwemo ya Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali kushirkiana na Mamlaka kuhakikisha kesi ambazo ziko mahakamani ushahidi unakamilika na kumalizika kwa haraka.
Kwa upande wake Kamishina Jenerali Gerald Kusaya ametumia nafasi hiyo kuelezea hatua kwa hatua mikakati inayofanywa na mamlaka hiyo katika kuendelea kupambana na dawa za kulevya na kwamba kumekuwa na mafanikio makubwa kutoka na kudhibiti mbinu zinazotumiwa na wanaojihusisha na biashara ya dawa hizo.
Aidha amesema maadhimisho hayo ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya kitaifa kwa hapa nchini yameanza leo na yanatarajia kumalizika kesho Julai 2,2022 ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atafunga maadhimisho hayo yaliyofunguliwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho hayo inasema hivi “Tukabiliane na changamoto za dawa za kulevya kwa ustawi wa jamii”.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala (wa tatu kushoto akiwa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupamba na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya (wa nne kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija(wa kwanza kushoto) pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa maofisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya baada ya kutembelea kwenye banda la mamlaka hilo lililopo kwenye Maadhimisho ya Kupinga matumizi ya dawa za kulevya ambayo kilele chake kinafanyika kesho Julai 2,2022 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja mkoani Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupamba na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya(wa kwanza kushoto) akipitia hotuba yake kabla ya kuisoma kwa wadau mbalimbali waliohudhuria kwenye Maadhimisho ya Kupinga matumizi ya dawa za kulevya yaliyoanza leo Julai 1 na yanatarajia kumalizika Julai 2,2022 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja mkoani Dar es Salaam.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi rasmi wa maadhimisho hayo.
Sehemu ya wanafunzi waliopata nafasi ya kutembelea viwanja vya Mnazi Mmoja wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa maofisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya wakati wa maadhimisho ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya yaliyoanza leo Julai 1 na yatahitimishwa kesho Julai 2 mwaka huu.Maadhimisho hayo kitaifa yanafanyika katika mkoa wa Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muriilo akiwa katika banda la Taasisi ya HJFMRI akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa taasisi hiyo kuhusu shughuli wanazofanya katika kukabiliana na mapambano ya vita za dawa za kulevya ikiwa pamoja na kutoa elimu kwa waribu walioathirika na utumiaji wa dawa za kulevya.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala (wa pili kushoto) akiwa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya( watatu kushoto) wakiwa katika Banda la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakipata maelezo ya mchango wa taasisi hiyo katika mapambano ya dawa za kulevya.
Mmoja wa maofisa kutoka Idara ya Uhamiaji akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala(katikati kushoto) akiwa na Kamishna Jeneral wa Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya.
Mmoja ya maofisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupamba na Dawa za Kulevya (kulia) akitoa maelezo kuhusu madhara ya dawa za kulevya na shughuli zinazofanywa na Mamlaka hiyo kwa mmoja ya wananchi waliofika kwenye banda hilo wakati wa maadhimisho ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya yaliyoanza leo Julai 1 na yanatarajia kumalizika kesho Julai 2,2022 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja mkoani Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakiendelea kuchukua machapisho mbalimbali yanayoelezea athari za matumizi ya dawa za kulevya baada ya kutembelea banda la Mamlaka ya Kudhibiti na Kupamba na Dawa za Kulevya.
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa maadhimisho ya dawa za kulevya yaliyoanza leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja mkoani Dar es Salaam.Ufunguzi wa maadhimisho ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya ambao umefanywa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala na kesho yatafungwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...