Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Kilimo Bwa. Joseph Kiraiya akizungumza katika  kikao cha majadiliano kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo kuhusu Mkakati wa Nchi wa AGRA TANZANIA katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wakifuatilia kikao kilichofanyika kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo kuhusu Mkakati wa Nchi wa AGRA TANZANIA katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.

 

Na Mwandishi wetu- Dodoma

SERIKALI imesema itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo kuhakikisha  inatatua changamoto zinazokabili sekta hiyo  ili kuwawezesha wakulima kufanya kilimo kinachoendana na teknolojia  kitakachosaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja  na kuchangia pato la Taifa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Kilimo Bwa. Joseph Kiraiya wakati akiongoza kikao cha majadiliano kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo kuhusu Mkakati wa Nchi wa AGRA TANZANIA katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.

Mkurugenzi huyo alisema  Programu ya kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) ni mpango wa miaka 10  unaolenga kuleta mageuzi ya sekta ya kilimo (Kilimo, Mifugo na Uvuvi), kuongeza uzalishaji wenye tija  na kufanya kilimo kuwa cha kibiashara.

“Mpango huu nia yake ni kuleta mageuzi kwa sekta hii kama tunavyojua ina mchango mkubwa sana katika pato la Nchi yetu hata wakulima kipato chao kitaongezeka, tutakuwa na chakula cha kutosha, usalama wa chakula na lishe,” alisema Mkurugenzi huyo.

Aidha Makamu wa rais anayesimamia Sera kutoka Shirika la Muungano wa Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA) Dkt. Nwafor Apollos alibainisha kwa shirika hilo liko tayari kufanya kazi na serikali katika kuboresha  mazingira ya kilimo nchini.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...