Na Said Mwishehe, Michuzi TV
SERIKALI imepokea vifaa aina ya Vishikwambi maarufu kwa jina la Tablet 200 kutoka UN Women zitakazotumika wakati wa Sensa ya Watu na Makazi inayotarajia kufanyika Agosti 23,2022 nchini Tanzania.
Akizungumza leo Julai 2, 2022 baada ya kupokea Tablet hizo Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Salum Kassim All amesema Sensa ya mwaka huu Serikali imejipanga kutumia mifumo ya kidigitali katika kudadisi kaya ambazo ziko katika maeneo yote.
“Udigitali huo vifaa ambavyo vimepangwa kutumika ni vifaa vya Vishikwambi au Tablet kwa lugha nyingine , tumekadiria kutumia vishikwambi 205,000 kwa ajili ya kutumika kwenye sensa ya watu na makazi nchini Tanzania.
“ Sasa hivi tumeanza kupokea vishikwambi kutoka maeneo mbalimbali na leo tumepokea vifaa hivi ambavyo tumevipata kutoka kwa wahisani, tumepokea tablet 200 vyenye thamani ya Dola za Marekani 85000 kutoka kwa UN Women.
“Na hivi karibuni tunatarajia kupokea vishiwambi vingine 10,000 kutoka Serikalini na mara kwa mara tutakuwa tukivipokea hadi kufikia idadi ambayo tunatarajia kuitumia wakati wa sensa,”amesema Mtakwimu huyo.
Akifafanua zaidi amesema uwepo wa vishikwambi na umuhimu wake vitarahisisha mchakato wa Sensa ya watu na makazi na wanategemea matokeo ya sasa yatapatikana mapema.
Kuhusu maandalizi ya sensa , amesema yanaendelea vizuri na wamefikia asilimia 87 na wanaelekea asilimia 90 za kukamilisha maandalizi.
“Jana Julai 1, 2022 tumefanya mafunzo ya wakufunzi katika ngazi ya taifa na hivi karibuni tunategemea kuwa na mafunzo ya ngazi ya pili itakayoanza mikoani kote Julai 6 na baadae mafunzo yataendelea Julai 28 kwa wale watakaodadisi katika maeneo yote ya Tanzania,”amesema.
Aidha amewaomba wananchi waaendelee kushiriki kwa kutoa ushirikiano kwa watakaokuwa kwenye jukumu la kudadisi katika maeneo husika.
“Lakini tulikuwa na ujumbe uliokuwa unasema tujiandae kuhesabiwa ila sasa hivi tunatakiwa kusema tushajiandaa kuhesabiwa tunasubiri siku ifike tuhesabiwe.
Kwa upande wake Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Mohamed Hamnza maandalizi yanakwenda vizuri na hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza mpaka sasa.
Aidha amesema umasishaji wa wananchi kushiriki kwenye sensa umekuwa ukifanywa na kada ya watu mbalimbali na jambo la kujivunia wananchi wamepokea kwa mikono miwili.
“Sensa ni yetu sote, hivyo kila mmoja anatakiwa kushajihisha kwa ajili ya zoezi hili la sensa ambalo kila mmoja anahusika nalo na jimabo la kitaifa,”amesema Balozi Hamnza.
Wakati huo huo Mwakilishi wa UN Women Tanzania Oldan Addou amesema wanatambua umuhimu wa sensa ya watu na makazi, hivyo wameona ni vema wakatoa vifaa hivyo ili kusaidia kufanikisha sensa hiyo.
Amesema taifa lolote linapojua idadi ya watu wake inakuwa rahisi kupanga mipango ya maendeleo huku akielezea Tablet ambazo wamekabidhi kwa Serikali zina thamani ya Dola za Marekani 85000.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Salum Kassim Ali (katikati) akiwa na Mwakilishi wa UN Women Tanzania (kulia) pamoja na Mwakilishi wa Finland(kushoto) wakiwa wameshika Tablet wakati yakifanyika makabidhiano leo Julai 2,2022.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar(wan ne kulia) akiwa na viongozi wengine pamoja na wawakilishi wa UN Women Tanzania na Mwakilishi wa Finland baada ya kufanyika tukio la kukabidhiwa kwa Tablet 200 ambazo zitakwenda kutumika katika sensa ya watu na makazi.
Mwakilishi wa UN Women Tanzania Oldan Addou(kulia) akielezea sababu za kuamua kutoa msaada wa Tablet hizo kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanikisha sensa ya watu na makazi ambayo mwaka huu itakuwa ya itatumia digitali zaidi kufanikisha sensa hiyo itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu.
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Zanzibar Balozi Mohamed Hamnza (kulia) akifafanua jambo kuhusu mwenendo wa maandalizi ya mchakato wa Sensa ya Watu na Makazi wakati wa tukuo la kukabidhiwa kwa Tablet.Kushoto ni Mwakilishi wa UN women Tanzania Oldan Addou.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Salum Kassim Ali(katikati) akikata utepe kama ishara ya kukabidhiwa rasmi Tablet ambazo zimetolewa na UN women .Wanaoshuhudia ni Mwakilishi wa UN Women Tanzania (kulia) na Mwakilishi wa Finland (kushoto).
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Salum Kassim Ali(kushoto) akiwa na Mwakilishi wa UN Women Tanzania Oldan Addou(kulia) wakiangalia moja ya Tablet baada ya kuifungua na kukabidhi kwa Serikali kwa ajili ya kusaidia kufanikisha sensa ya watu na makazi.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Salum Kassim Ali(katikati) akisisitiza jambo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...