Njombe
WATU
wanne wamenusuriko kifo mara baada ya bajaji namba MC 567 CJK aina ya
TVS iliyokuwa ikitoka maeneo ya stendi kuu ya mji wa Njombe kuelekea
katikati ya mji kupinduka kutokana na mlipuko mkubwa wa simu ya abiria
uliosababisha moto.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema bajaji hiyo imepinduka
kutokana na dereva kugeuka nyuma kutokana na taharuki ya kulipuka kwa
simu ndogo mali ya Siston Antony katika barabara kuu ya Njombe-Songea
majira ya saa tano asubuhi.
“Moto
umelipuka mkubwa na dereva wa bajaji akageuka kuangalia abiria wake na
kushindwa kuiongoza akaiachia bajaji wakapinduka”amesema Kamanda Issah.
Kamanda
Issah amesema baada ya ajali hiyo polisi imeweza kuingilia kati
kutokana na mmiliki wa bajaji kutaka kulipwa na abiria mmiliki wa simu
iliyosababisha mlipuko na kupelekea kupinduka kwa bajaji na kuharibika.
Aidha
Kamanda Issa ametoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya moto kuwa na bima
za vyombo vyao ili kuepusha usumbufu kama huo huku pia akitoa rai kwa
wamiliki wa simu kuwa makini na matumizi ya simu zao,na kubainisha kuwa
abiria wote waliweza kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu ya
majeraha madogo na kuruhusiwa kutoka ili kuendelea na shughuli zao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...