SHIRIKA  la Madini la Taifa STAMICO limeanza rasmi kupeleka kwa wananchi bidhaa  yao ya mkaa mbadala na rafiki wa makaa ya mawe kwa ajili ya kuanza kutumika kwa matumizi ya nyumbni ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha sera ya uhifadhi inatekelezwa kwa vitendo.

Akizungumza leo Julai 1,2022 katika maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaa meneja Masoko na Uhusiano wa STAMICO Geofrey Meena amesema kwa sasa Bidhaa hiyo imeeanza kuuzwa na kwamba mpaka sasa tayari wameshapokea maombi mbalimbali ya mawakala kwaajili ya kusambaza bidhaa hiyo nchi nzima.

Amesema wapo kwenye maonesho hayo ya  Sabasaba na bidhaa yao ya mkaa  mbadala pamoja na mambo mengine, lakini wanataka  kuwaeleza wananchi kuwa sasa bidhaa hiyo inapatikana hapa kweye maonesho. “uzalishaji unafanyika katika kiwanda chetu kilichopo TIRDO Msasani na tunaenda kuandaa utaratibu wa kuwapata mawakala watakaosambaza mkaa huu nchi nzima" amesema

Ameongeza kwamba  "Mkaa huu ni mkombozi kwa wananchi kwani unweza kutumika kidogo kwa matumizi ya siku nzima na utasaidia sana kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na kukatwa misitu " ameongeza.

Aidha amesema kuwa katika maonesho ya mwaka huu STAMICO wamekuwa na banda lao wao wenyewe ikishirikiana na baadhi ya Taasisi kutoka Sekta Binafsi zinazojihusisha na uchimbaji wa Dhahabu pamoja na kiwanda cha kusafisha Dhahabu kiichopo Jijini Mwanza.

Amezitaja Taasisi zilizoshirikiana na na STAMICO katika maonesho hayo ni pamoja na Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ya Buckreef Mining Company, Buhemba Gold Mining na Kiwanda cha Mwanza Precious Metals refinery Limited cha Jijini Mwanza.

Kwa upande wake Mhandisi Mtaalamu Uchenjuaji Mandini kutoka STAMICO Happy Mbenyange anayesimamia Bidhaa hiyo amesema kuwa uzalishaji wa Bidhaa hiyo unakwenda vizuri ambapo kwa sasa mtambo wao una uwezo wa kuzalisha tani mbili kwa saa na kwamba wanatarajiwa kupokea mitambo mingine kwaajili ya kuongeza uzalishaji wa Bidhaa hiyo.

Pia amesisitiza kuwa Bidhaa hiyo ipo kwa wingi hivyo wananchi wanaweza kufika kwenye maonesho hayo kujipatia Bidhaa hiyo kwa bei nafuu.

"Mkaa upo wa kutosha na unapatikana hapa sabasaba wananchi wanaotembelea Maonesho haya wafike kwenye Banda letu la STAMICO kupata Bidhaa hii kwa bei nafuu" amesema happy.

Deus Magala Mkurugezi Rasilimali Watu shirika la Madini Tanzania STAMICO akisisitiza jambo wakati akizungumza na baadhi ya watu waliofika kwenye banda la hilo katika maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam
Deus Magala Mkurugezi Rasilimali Watu shirika la Madini Tanzania STAMICO akizungumza na baadhi ya watu waliofika kwenye banda la hilo katika maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo Ijumaa 1,2022 wa pili kutoka kulia ni Mhandisi Mchenjuaji Madini STAMICO Bi. Happy Manyange na kushoto ni Mhandisi Pili Athumani.
Mwalogo Ofisa  kitengo cha tehama Shirika la Madini Tanzania STAMICO akizungumza na Bi. Happy Manyange Mhandisi Mchenjuaji Madini STAMICO.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...