Na Janeth Raphael - Chemba, Dodoma
TAASISI ya Benjamini Mkapa(BMF) kupitia mradi wa ‘Mkapa Fellow’ awamu ya tatu, imetajwa kusaidia kuondoa vikwazo vya upatikanaji wa huduma rafiki kwa vijana Wilaya ya Chemba, mkoani Dodoma.

Miongoni mwa vikwazo hivyo ni pamoja na kukosekana kwa elimu ya uzazi wa mpango, kujikinga na Virusi vya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na ukatili wa kijinsia kwa vijana.

Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk.Marko Mgonja aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi huo unaofadhiliwa na Serikali ya Ireland kupitia mfuko wa Irish Aid ikiwa ni kuelekea jukwaa la kumbukizi ya pili ya aliyoyafanya na kuacha alama Muasisi wa taasisi hiyo, Hayati Rais Benjamini Mkapa, litakalofanyika Julai 13 – 14 visiwani Zanzibar.

Alisema kupitia mradi huo Halmashauri imeongeza idadi ya vituo vinavyotoa huduma rafiki kwa vijana kutoka 10 hadi 35 ambapo wamekuwa wakielimisha masuala ya uzazi wa mpango na matumizi ya kondomu ili kujiepusha na maambukizi ya VVU.

“Katika kipindi cha Disemba-Februari 2022 ni vijana 316 tu walipata huduma za masuala ya uzazi lakini katika kipindi cha mwezi Machi hadi Mei 2022, jumla ya vijana 1,135 (359%) walipata huduma hizo,”alisema.

Kwa upande wake, Ofisa Miradi Mwandamizi wa Taasisi hiyo, Daudi Ole Mkopi, amesema taasisi hiyo imekuwa ikifanya kazi ya kuimarisha mifumo ya sekta ya afya kwa jamii.

“Katika kuhakikisha jamii hususani vijana wanapata elimu sahihi na kutafuta huduma hizo katika vituo vya kutolea huduma kwa wakati, BMF imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na vijana kundi balehe ili kufikisha ujumbe katika jamii wanayoishi,”alisema.

Alisema kuwa mradi huo umesaidia hadi sasa vijana wameunda makundi 30 yenye wanachama 395 ambapo wamekuwa wakikutana mara moja kila wiki kujadili masuala ya afya.

“Hawa waelimishaji rika wameweza kuwafikia vijana wenzao wapato 2,483 na kutoa elimu mbalimbali kama vile matumizi sahihi ya kondomu,elimu ya afya ya uzazi, magonjwa ya ngono, ukatili wa kijinsia, elimu ya lishe na madawa ya kulevya pindi wanapotembelea kaya na kwenye mikutano ya hadhara,”alisema.

Pamoja na hayo, Afisa mwandamizi huyo amesema katika kukabiliana na vikwazo vya kiuchumi vinavyosababisha vijana kujiingiza kwenye tabia hatarishi vijana hao wamebuni miradi ya maendeleo na ujasiriamali.

  "Ndani ya miezi mitatu vikundi 18 vimeanzisha shughuli za ufugaji wa kuku,sungura,nguruwe,kilimo cha mboga, alizeti na ushonaji wa nguo"

Naye, Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya hiyo, Verdiana Joseph, alisema mradi huo umefanikiwa kuwaondoa vijana kwenye makundi hatarishi ikiwamo kundi la vijana lililojiita Maronjo ambalo lilikuwa linajihusisha na ubakaji.

“Pamoja na kukamatwa kamatwa lakini pia kwasasa vijana ambao ni miongoni mwa kundi hilo wameacha tabia hizo na sasa wanajishughulisha na miradi ya kilimo cha mboga na ufugaji wa kuku,”alisema.

Saidatu Omar ni mwelimishaji rika katika Wilaya hiyo ya Chemba zahanati ya Nondo amesema anaishukuru Taasisi ya Benjamin Mkapa Kwa kuwapatia mafundisho ya elimu ili na wao waweze kuelimisha Vijana wenzao 

" Tumeanzisha vikundi mbalimbali na miradi inayotukeamua kimaisha"

Taasisi ya Benjamin William Mkapa Foundation Kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeandaa kongamano la kumbukizi ya pili litakalofanyika tarehe 13-14 mwezi huu, 2022 katika ukumbi wa hotel ya golden tulp Zanzibar na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chemba Dkt Marko Mgonja akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi huo unaofadhiliwa na Serikali ya Ireland kupitia mfuko wa Irish Aid ikiwa ni kuelekea jukwaa la kumbukizi ya pili ya aliyoyafanya na kuacha alama Muasisi wa taasisi hiyo, Hayati Rais Benjamini Mkapa, litakalofanyika Julai 13 – 14 visiwani Zanzibar.
Ofisa Miradi Mwandamizi wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa Foundation Dkt Daudi Ole Mkopi akizungumza kuhusu taasisi hiyo imekuwa ikifanya kazi ya kuimarisha mifumo ya sekta ya afya kwa jamii.
Muelimishaji rika kutoka zahanati ya Nondo Wilaya ya Chemba Saidatu Omar akiishukuru Taasisi ya Benjamin Mkapa kwa kuwapatia mafundisho ya elimu ili na wao waweze kuelimisha Vijana wenzao 
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...