Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma imefanikiwa kukusanya ufuta zaidi ya tani 2300 kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Ghala la Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru (TAMCU) Sarah Chirwo wakati anatoa taarifa ya ununuzi wa ufuta kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani kwa Mkurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Mfumo wa stakabadhi ghalani nchini Asangye Bangu mjini Tunduru.

Amesema tani zilizonunuliw ni hadi kufikia Julai 16 mwaka huu na kwamba ukusanyaji wa ufuta bado unaendelea kwa kasi kubwa ambapo wakulima wanafurahia mfumo huo kwa sababu wanauza mazao yao kwa bei nzuri.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru Musa Manjaule amesema wakulima wa Tunduru wameelewa faida za mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umemaliza kero ya muda mrefu ya kuibiwa kupitia mfumo holela wa kununua mazao.

“Sisi Tunduru ukituambia stakabadhi tuitoe hatuwezi kukuelewa,kwa sababu tunajua ubaya wa Mfumo holela wa kununua mazao”,alisema Musa.

Kwa upande wake Mkulima Rajabu Mohamed Mkazi wa Ligunga Tunduru amesema licha ya kujitokeza wakati fulani changamoto ya kuchelewa malipo,bado mfumo wa stakabadhi ghalani una faida nyingi kuliko hasara.

Akizungumza baada ya kusikiliza kero za wakulima Wilaya Tunduru,Mkurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Mfumo wa stakabadhi ghalani nchini Asangye Bangu ameahidi kushughulikia changamoto hizo ikiwemo ya kuchelewa kwa malipo na pembejeo za kilimo.

Katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Mfumo wa stakabadhi ghalani ameongozana na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania,Mrajis wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Ruvuma,Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mtendaji Mkuu toka Wakala wa Vipimo na Mwakilishi wa Kituo cha Utafiti wa Mazao TARI.

Mkurugenzi huyo anatembelea Wilaya zote ambazo zinanunua mazao kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wakulima na kuzitafutia ufumbuzi.

MAELEKEZO YA picha zote zinaonesha ufuta ambao umekusanywa katika ghala kuu la Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru TAMCU ambapo hadi sasa wamefanikiwa kukusanya zaidi ya tani 2300


Anayezunguma katika picha ni Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru TAMCU Sarah Chirwo akitoa taarifa ya ukusanyaji wa zao la ufuta kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...