Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
MKURUGENZI wa Mji wa Gaita ambaye pia ni Mlezi wa Timu ya Gaita Gold FC, Mhe. Zahara Michuzi ameahidi kuwa msimu ujao wa mashindano watahakikisha wanapambana na kufanya vizuri katika Ligi Kuu Soka Tanzania Bara na Mashindano mengine ambayo timu hiyo inashiriki kwa kuandaa Kikosi bora chenye ushindani.
Zahara Michuzi ameyasema hayo wakati wa utoaji wa Tuzo za ‘NBC, TFF Awards’ unaofanyika jijini Dar es Salaam, wakati akipokea Tuzo ya Mshindi wa Nne katika Ligi Kuu (NBC Premier League) msimu wa 2021-2022.
“Msimu ujao tunaahidi tutagawana vikombe kwenye mashindano ya hapa nyumbani kwa maandalizi tunayoenda kufanya Geita Gold FC”, amesema Zahara.
Zahara Michuzi amesema Geita Gold FC na Uongozi wake wanatekeleza agizo la Serikali kwa asilimia 100%, agizo linalotaka kila timu kuwa na uwanja wake kama Sera ya Michezo inayoelekeza. Amesema hadi sasa wanatekeleza agizo hilo kwa ujenzi wa uwanja wao unaojengwa eneo la Magogo ambao umefikia asilimia 85%.
“Sisi Geita Gold FC, tunatekeleza agizo la Serikali kwa kujenga uwanja wetu wa kisasa, na pia tunaedelea kutoa fursa mbalimbali za ajira kuajiri watu mbalimbali kwenye maeneo mbalimbali kwenye Klabu yetu”, amesema Zahara Michuzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...