Na. WAF – Mtwara

Watumishi wa Hospital ya Rufaa Kanda ya Kusini Mtwara kujengewa nyumba 20 vya malazi pamoja na kununuliwa magari mawili (Coster) na Gari kwa ajili ya Mkurugenzi ili kuwasaidia kutekeleza majukumu yao vizuri.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameyasema hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brig. Gen Marco Gaguti leo Julai 24, 2022 baada ya kufanya ziara katika hospitali hiyo kwa lengo la kuangalia maendeleo ya ujenzi wa vyumba mbalimbali vya kutolea huduma ya Afya kwa wagonjwa.

“Nimefurahi sana kuona hospitali hii imefika katika hatua hii baada ya kutelekezwa takribani miaka 30, namshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutugawia fedha takriban zaidi ya Bil. 10 kwa kutekeleza ahadi yake ya kuendeleza miradi yote iliyoanza miaka mitano iliyopita.” amesema Waziri Ummy

Waziri Ummy amesema awamu ya tano iliwekeza kwenye majengo na sasa awamu ya sita inawekeza kwenye vifaa ambavyo vimepatikana katika hospitali hiyo ni pamoja na MRI, CT-Scan, ufungwaji wa Digital X-ray mashine mbili, Mobile digital X-ray mbili, Ultra-Sound mbili na vifaa vingine.

Aidha, Waziri Ummy amewataka wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanawalipa stahili zao watumishi wote wapya wa Afya kwa wakati ili waweze kurudi haraka kwa kuwa kuna wengine hawajaingizwa kwenye mfumo wa malipo (Payroll).

“Naomba watumishi wote nchini ambao mmeenda kuripoti katika vituo vyenu vipya vya kazi baada ya siku 14 mrudi katika maeneo yenu ya kazi, na Tunafurahi kwakuwa wengi mmeripoti. ” amesema Waziri Ummy

Pia, Waziri amewataka watumishi wote kishirikishana katika utendaji wao kwa kuwa lengo la pamoja ni kuhakikisha huduma bora inatolewa kwa wagonjwa.

Hata hivyo, Waziri Ummy amesema ataunda bodi ili waweze kuisimamia hospital hiyo ya Rufaa kanda ya kusini-Mtwara kwa kuweza kujiendesha yenyewe.

Katika ziara hiyo Waziri Ummy aliambata na viongozi wengine kutoka wizara ya Afya pamoja na viongozi kutoka katika Mkoa wa Mtwara wakiongozwa na mkuu wa Mkoa huo Brig. Gen. Marco Gaguti



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...