Na Mwandishi Wetu, Chamwino.

ZAIDI ya vikundi 32 vya Sanaa ya ngoma vinatarajia kushiriki Tamasha la msimu wa 13 la muziki wa Wagogo (Cigogo Music festival),litakalofanyika Julai 23-24, Chamwino.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sanaa Chamwino (Chamwino Arts Center- CAC), Bw. Frank Mgimwa, alibainisha kuwa, tayari maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa,Mgimwa amevitaja vikundi hivyo kuwa, ni pamoja na:

"Kikundi cha: Nyota Njema, Sinai, Nyerere, Yeriko,Chibibi, Ushirikiano na Yerusalemu vyote kutoka Wilaya ya Chamwino.

Vingine ni: Nyota Njema na Ndagwa vyote kutoka Msanga, pia kundi la Mama Jusi (Chilonwa), Mch.Mwema (Nzali), Jembe (Bwawani/Chalinze), Nuru (Mlebe), Mwenda pole (Buigiri),

Pia vipo Juhudi, Tumaini (Kawawa), Inueni mioyo (Msamalo), Safina (Msanga), Ufunuo (Mlimwa), Nyemo (Mapanga), Dudu Baya (Chilonwa), Sayari (Membe), Swala (Mkoyo), Faru (Songambele), Nyota Lamali (Majeleko),

Vikundi vingine ni Nyati (Nzali), Muungano (Singida), Kipauli-Njombe (Njombe), Hiyali ya moyo (Dodoma Jiji), Afrika Bati (Morogoro), Fountain Gate Academy (Dodoma Jiji), na Ilula (Iringa).

Aidha, amesema kuwa, vikundi hivyo vitapamba kwa burudani mbalimbali kwa siku zote mbili.

"Hadi kufikia Julai 22, 2022 vikundi vyote vitakuwa vimefika hapa Chamwino Ikulu Vijijini,Na Tamasha litapamba moto kwa siku mbili, Julai 23-24, watu wote wanakaribishwa hakuna kiingilio, ni bure." Alisema Mgimwa.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...