Na. Fred Shirima/Serengeti


Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana alitembelea Hifadhi ya Taifa Serengeti leo 23/07/2022 na kupata maelezo juu ya kituo cha kutoa habari kidijitali (Serengeti Media Center) kinavyofanya kazi ya kutangaza vivutio, shughuli za hifadhi na za jamii zinazozunguka hifadhi hiyo.

Dkt. Chana amepongeza TANAPA kwa kazi nzuri inayofanya na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya hifadhi na shirika kwa ujumla.

Awali, Dkt. Chana alikutana na Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa Serengeti ambapo Mkuu wa Hifadhi hiyo Kamishna wa Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Izumbe Msindai alitoa taarifa fupi kuhusu hifadhi

Naye, Kamishna wa Uhifadhi - TANAPA, William Mwakilema alimshukuru Waziri Chana kwa kutenga muda na hasa kutembelea maeneo haya ili kujionea shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii zinavyofanyika.

Kituo cha Serengeti Media Centre (SMC) kimeshaanza kufanya kazi na watalii wameanza kukitumia kupata taarifa mbalimbali za hifadhi na kinatarajiwa kufunguliwa rasmi hivi karibuni.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...