Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
WAKAZI
wa Vitongoji vya Kata ya Kisutu, Jimbo la Bagamoyo ,Mkoa wa Pwani,
wamemtaka mbunge wa Jimbo hilo Muharami Mkenge kuendelea kusimamia na
kuzifikisha kero zao kwenye Mamlaka husika ili zipatiwe ufumbuzi ikiwa
ni pamoja na kero ya umeme, maji , miundombinu mibovu ya barabara na
fedha za Mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF).
Wakitoa
kilio cha changamoto hizo, wakati wa mkutano na mbunge huyo , baadhi ya
wakazi akiwemo Farida Ramadhani,Matuka Mnyimadi walisema shule
imejengwa, Lakini bado wana kero ya barabara Na hawajasajiliwa kipindi
kirefu wanachama wapya katika TASAF.
Chrisantus Joseph amemuomba mbunge kuingilia kati kero ya ushuru wa mafuta katika Bandari ya Bagamoyo.
Akizungumza
na wakazi hao , Muharami Mkenge alieleza, Serikali inaendelea na juhudi
za kuwapatia maendeleo wananchi wake kwa awamu .
Aliwaomba
wananchi kuvuta subira wakati Serikali ikiendelea kutatua kero za maji,
barabara na umeme kwenye Maeneo ambayo bado hayajafikiwa.
"Serikali
ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu imetekeleza mengi
kwenye sekta na nyanja mbalimbali ya maji, barabara za mijini na
Vijijini,umeme ambapo inaendelea kuongeza kutenga fedha nyingi hususan
bajeti mpya ya 2022/2023 ili kutatua kero zilizopo".
Aidha
Mkenge amezungumzia mradi mkubwa wa barabara unaotarajia kutekelezwa
ambapo, sisi Bagamoyo tumeomba tujengewe barabara ndani ya mji,
mifereji, lambo na mambo mbalimbali," alisema Mkenge.
Mkenge
pia aliwasihi wananchi kujitokeza katika Zoezi la sensa agost 23 mwaka
huu kila mmoja ashiriki bila kukosa,kwani itasaidia kuweka mipango
mizuri ya kimaendeleo kwa kuwa na idadi kamili ya watu na makazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...