Na. James K. Mwanamyoto-Babati
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema watumishi wa umma nchini wana deni kubwa la kutoa huduma bora kwa wananchi, kwasababu Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameboresha masilahi yao ili kujenga ari na morali ya kulitumikia taifa.

Mhe. Ndejembi amesema hayo, wakati akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Mji Babati, akiwa katika ziara ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamozo zinazowakabili watumishi wa umma katika Halmashauri hiyo.

“Watumishi wa Halmashauri ya Mji Babati mmeona namna Mhe. Rais alivyowapandisha madaraja na alivyolipa malimbikizo yenu ya mishahara, hivyo mna deni kubwa kwa Mhe. Rais la kufanya kazi kwa uadilifu pamoja na kutoa huduma bora kwa Watanzania,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa, Serikali kazi yake kubwa ni kutoa huduma kwa wananchi, hivyo watumishi wa umma wa Halmashauri ya Mji Babati pamoja na wa maeneo mengine wameajiriwa ili kutekeleza azma hiyo ya Serikali na si kufanya biashara.

Akizungumzia changamoto ya utendaji kazi wa baadhi ya watumishi wa umma nchini, Mhe. Ndejembi amesema baadhi yao wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea bila ya kuwa na mpango kazi hivyo kushindwa kutoa huduma bora kwa wananchi kama ambavyo Serikali imekusudia.

“Wengi wetu hapa hatuna mpango kazi, tunafanya kazi kwa matukio wakati shida za wananchi ni nyingi sana na tunao wajibu wa kuzitatua kwa wakati kwa kuwa na mpango kazi unaotekelezeka,” Mhe. Ndejembi ameongeza.

Kwa upande wake, Mbunge wa Babati Mjini, Mhe. Pauline Gekul ambaye pia ni Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo amemshukuru Mhe. Ndejembi kwa kufanya ziara ya kikazi jimboni kwake kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi walio katika jimbo lake ambao ndio watekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mhe. Gukul amesema, kazi inayofanywa na Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wake Mhe. Deogratius Ndejembi ya kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma nchini, inaongeza ari ya utendaji kazi kwa watumishi wa umma ambao wana jukumu la kumsaidia Mhe. Rais kutoa huduma bora kwa wananchi.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Halmashauri ya Mji Babati ya kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika halmashauri hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mji Babati (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi katika halmashauri hiyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Mji Babati wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi katika halmashauri hiyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.
Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Babati, Mhe. Lazaro Twange akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mji Babati wakati wa ziara yake ya kikazi katika halmashauri hiyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi.
Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Mji Babati, Bw. Nemes Fungameza akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Halmashauri ya Mji huo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya Mji Babati, Bw. Faraja Maduhu (aliyesimama) akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi (katikati) akisikiliza hoja iliyokuwa ikiwasilishwa na mtumishi wa Halmashauri ya Mji Babati wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi.
Mtendaji Kata wa Kata ya Sigino Halmashauri ya Mji Babati, Bi. Evaline Panga (aliyesimama) akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...