Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Halfan Ramadhan, akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Mafuta na Gesi, Robinnancy Mtitu, uzalishaji wa mafuta na gesi wakati wa Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.


WAKATI Tanzania ikitarajia kuvuna neema ya gesi asilia katika mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia(LNG), kampuni za wazawa zimeshukuru na kuipongeza serikali kwa kuwapa fursa ya wao kunufaika na mradi huo.

Wakizungumza na vyombo vya habari leo Julai  9 2022, katika maonyesho ya 46 ya biashara ya kimataifa Dar es Salaam (DITF)  kwenye banda la Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), walisema kuwa wameona thabiti ya serikali katika kuhakikisha wazawa wananufaika kwenye fursa mbalimbali zinazojitokeza katika sekta hiyo ikiwamo Mädel mkubwa wa LNG.

Halfan Halfani ni Mwenyekiti wa bodi ya PURA, amesema kuwa mradi wa LNG, utasaidia kuongeza ajira kwa watanzania ambapo watu takribani elfu kumi wanatarajiwa kupata ajira hizo.

Amesema kuwa kwenye mradi huo wafanyakazi wasiopungua  500, watapata kazi na kwamba katika eneo hilo la mradi kutakuwa na ajira nyingi kwa watu wa bodaboda, mama ntilie pamoja na wajasiriamali wengine wa aina mbalimbali

“Mradi huu wa NLG utakuwa na tija kwa taifa kwani utadumu kwa zaidi ya miaka 50 huku tukitarajia kupata manufaa mara mbili, kwanza hela tutakayopata kwa kuuza gesi ambayo itakuwa ikiuzwa mpaka nje ya nchi na kupata fedha za kigeni na pia kwa kufanikisha nishati  kwa viwanda, nyumba, magari na Taasisi za hapa nyumbani na hivyo kutusaidia kufanya uzalishaji wa ndani” amesema Halfani.

Frank Mwankesi ni Mfanyakazi wa  chama cha wafanyakazi cha mafuta na gesi (OGAOGA) ameipongeza serikali kwa kuweka  mazingira wezesha ya ajira katika sekta ya madini na gesi.

Tumaini Abdallah ni mmoja wa vijana wanaofanyakazi kwenye Kampuni za kizalendo zitakazonufaika na mradi wa LNG, ametoa shukrani kwa Pura kwa kuziamini kampuni za ndani za uchimbaji wa gesi na mafuta na hivyo kuaminika kwa Kampuni za kigeni zinazokuja kutekeleza uchimbaji  wa gesi asilia mkoani Lindi.

 Tumaini ametoa wito kwa Vijana wa Kitanzania kujitokeza kwa wingi kwenye fursa hiyo kwa kuwa serikali ipo tayari kuwapa nafasi.

“Vijana msiogope msaada upo na serikai ipo kwa ajiri yetu kama ambavyo sisi tumenufaika kwenye mradi huu,"anasema Tumaini

Tumaini Abdalah akizungumza  na waandishi wa habari hawapo wakati alipotembelea banda ya PURA kwenye wa Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Halfan Ramadhan, akizungumza  na waandishi wa habari hawapo wakati alipotembelea banda ya PURA kwenye wa Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa, Dar es Salaam
Frank Mwankesi,  akizungumza  na waandishi wa habari hawapo wakati alipotembelea banda ya PURA kwenye wa Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...