Wazazi wamehimizwa kuwapeleka watoto wao kwenye taasisi za elimu zinazotoa elimu ya vitendo ili kuwajengea uwezo binafsi wa kujiajiri baada ya masomo. Wosia huu ulitolewa na Mbunge wa viti maalumu Bahati Keneth Ndingo kwenye mahafali ya wanafunzi wa kilimo kutoka chuo cha Kaole Wazazi kilichopo Bagamoyo.
Mahafali haya yaliyofanyika ni ya sita kwa chuo hiki kwa wanafunzi wanaosoma ngazi ya kilimo na mifugo.
Ndingo alinukuliwa, ‘nawaasa wazazi wahakikishe vijana wao wanapata elimu endelevu itakayowasaidia kufanya vizuri hata baada ya kumaliza vyuoni. Uwekezaji wa elimu ulenge kuwapa uwezo binafsi wa kuwasaidia wengine pia kujikwamua kimaisha’.
Aidha, mkuu wa chuo cha Kaole, Sinani Simba nae alisema, ‘wanafunzi hawa wana ubobezi mzuri sana kwenye fani zao hizo mbili na wana weledi wa kutosha kutokana na mafunzo ambayo waliyoyapata hapa chuoni’.
Aliendelea, ‘wanafunzi wanaohitimu ni 122 kati ya hao 24 wanahitimu stashahada ya kilimo na 33 stashahada ya kilimo na 65 ni stashahada ya afya na uzalishaji wa mifugo’.
Kwa hivi sasa chuo cha Kaole kinafundisha wanafunzi wanaohitimu astashahada na stashahada za kilimo na mifugo. Pia chuo kina wanafunzi waliothibitishwa na (National council for technical and vocational education training (NACTVET) wanaosoma masomo ya kilimo na mifugo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...