Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAZIRI  wa Afya Ummy Mwalimu ametembelea Banda la Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba(TMDA) lililopo katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba mkoani Dar es Salaam ambapo amefurahiswa na Mamlaka hiyo kushiriki maonesho hayo.

Amefurahiswa na utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu ubora , usalama na ufanisi wa bidhaa za dawa,vifaa tiba pamoja na vitendanishi lakini kubwa zaidi ambalo Waziri wa Afya ni  baada ya kuona namna gani wanatoa elimu kuhusiana na madhara yanayotokana na matumizi ya bidhaa za tumbaku.

Kingine ambacho Waziri Ummy Mwalimu amefurahiswa ni kuona TMDA inajipanga katika kuhakikisha masuala mazima ya kutoa elimu hususani katika kueleza kemikali ambazo zipo katika bidhaa za tumbaku na katika kuelezea wamekuwa wakionesha kemikali za sumu ambazo zinapatikana kwenye tumbaku.

Hivyo amefurahi kuona Wananchi wanapata uelewa kwasababu suala zima la matumizi ya tumbaku linahitaji mtu awe na uelewa anapoingia katika matumizi yale ajue kabisa nini matokeo yake.

Akiwa katika banda hilo, maofisa wa TMDA wakiongozwa na Mkurugenzi wao Adam Fimbo wamemueleza Waziri kuwa wamekuwa wanahusisha wadau ambao wanamiliki maeneo ya wazi  kuzingatia yale yanayotakiwa kufanyika kwa maana ya kutenga eneo maalum ya uvutaji lakini waweke alama za kuonesha No Smoking na Smoking area.

Lengo la kufanya hivyo ni kumkinga asiyetumia na wanaotumia wajue nini kitatokea kutokana na matumizi ya tumbaku.Waziri Ummy ambaye alikuwa ameambatana na Mratibu wa Kimataifa wa Mapambano ya UVIKO-19 kutoka Umoja wa Mataifa Dk .Ted Chaiban ambapo naye ameonesha kufurahia hatua zinazochukuliwa na TMDA katika kuelimisha umma kuhusu usalama na ubora wa dawa na vifaa tiba.




Matukio mbalimbali katika picha baada ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kutembelea Banda la Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) akiwa ameambatana na Mratibu wa Kimataifa wa Mapambano ya UVIKO-19 kutoka Umoja wa Mataifa Dk.Ted Chaiban.Wakiwa katika banda hilo wamepokelewa na maofisa na Mkurugenzi wao mkuu Adam Fimbo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...