Na Mwandishi Wetu
WAKALA wa Vipimo Tanzania (WMA)umebainisha uwepo wa vituo zaidi ya 5000 nchi nzima kwa ajili ya kufanya ukaguzi ili kuendelea kuhakikisha Mtanzania anapata bidhaa ambayo iko kwenye ujazo na Vipimo vinavyostahili huku ikiendelea kuwabaini Wafanyabishara wanaofanya udanganyifu.
Akizungumzia na waandishi wa habari katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba mkoani Dar es Salaam Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) Stella Kahwa amesema kuwa Wakala huo umejipanga vema katika kuwatumikia Watanzania.
Amefafanua kupitia vituo hivyo kumeleta matokeo chanya na kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili walaji na kwamba kwa sasa wengi wao wanafanya biashara zao kwa kufuata taratibu zilizopo.
"Kwa sasa Changamoto hii imepungua kwa kiasi kikubwa kwa sababu tunapoenda kufanya kaguzi hatukutani na waliokiuka taratibu hata wale wanaopigwa faini wamepungua sana hadi kufikia asilimia 80 na 85" amesema.
Aidha ameendeleakutoa mwito kwa wafanyabiashara na walaji kwa ujumla kuendelea kufuata taratibu zilizopo ili kila mmoja aweze kunufaika. Pia amewakaribisha wananchi wote hususani wafanya Biashara kufika kwenye Maonesho ya sabasaba na kutembelea Banda lao ili kujifunza na kufahamu namna Taasisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria.
"Nawaambia wafanyabiashira waje hapa sabasaba wajionee namna ambavyo wakala wa vipimo inavyofanyakazi, Wakala wa Vipimo iko Juu hivi sasa" alihitimisha Kahwa.
Kwa upande wake Ofisa Vipimo Mkuu WMA Gaspar Matiku amesema kuwa kwa sasa WMA imejipanga kuhakiki vipimo kwenye gari ndogo za biashara (tax) kwa kufunga tax meter ambazo zitasaidia kufahamu mteja ametembea kwa umbali fulani na kuweza kulipa fedha halali ambayo inalingana na umbali aliotembea.
Amesema kwa kufanya hivyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kujua umbali na fedha ambayo inatakiwa kulipwa na mteja kutokana na umbali uliotumika.“Biashara ya Tax imekuwa kubwa na inatumika, sasa badala ya mtu kutamkiwa kwamba unatoka hapa ninakwenda sehemu fulani, huyu anakumbia utanipa elfu 20 na mwingine anakuambia utanipa elfu 30 kwa hiyo hakuna usawa kwenye hiyo ruti."




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...