Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi
akisalimiana na Viongozi wakati alipowasili viwanja vya ukumbi wa Chuo
cha Utalii Maruhubi Wilaya ya Magharibi”A” wakati akianza ziara yake ya kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo.[Picha na Ikulu] 16/07/2022.
Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi na Serikali wakiwa katika hafla
ya usomwaji wa Ratiba ya ziara ya Rais wa Zanziar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi aliyoianza leo kwa kutembelea
miradi ya maendeleo katika maeneo ya Shehia mbali mbali za Wilaya ya Magharibi”A”huko katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akisoma kitabu cha ratiba iliyokuwa ikisomwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Idrissa Kitwana Mustafa (hayupi pichani) katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi leo kabla ya kuanza ziara katika Wilaya ya Magharibi”A” ya kutemelea na kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la
kujenga Uchumi JKU Kanali Makame Abdalla Daima kuhusu Ujenzi wa Skuli ya
Kihinani Msingi iliyojengwa na Kikosi chake Ujenzi wa madarasa kumi na mbili kupitia fedha za UVIKO 19, wakati wa ziara ya kutembelea na kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (wanne kulia)alipokuwa akisoma maandishi
ya jiwe la msingi Hospitali ya Wilaya Mbuzini mara ya kufungua pazia
jiwe hilo ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa Hospitali hiyo leo akiwa
katika ziara ya kutemelea na kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo kwa Wilaya ya Magharii “A”.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa pili kushoto) alipokuwa akizungumza
na Wajenzi wa Kampuni ya Ujenzi wa Tangi la Maji Safi na Salama “Mehga
Ingeneering &Instruction LTD “ambayo imeahidi
kumalizika kwa ujenzi huo ifikapo Mwezi januari Mwakani,wakati wa ziara
ya kutemelea na kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akimsikiliza Bibi Raifa
Kibwana Mkaazi wa Dole, Wilaya ya Magharibi A akizungumzia changamoto
zinazowakabili katika Shehia yao wakati wa ziara ya kutembelea na kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi
alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Mwera wakati alipozindua ujenzi wa
Barabara za Vijijini kwa kiwango cha lami,alianzia barabara ya Mwera
-Kibondemzungu wakati wa ziara ya kutemelea na kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto )alipokuwa akisisitiza jambo
wakati alipoisimamisha kazi Kampuni ya Assosiated Investiment&
Services LTD ya Dar Es Salaam chini ya usimamizi wa Nd,Theodony Andrew Zani kutokana na utendaji wao wakazi wa kusuasua katika Shehia ya Monduli akiwa katika ziara ya kutembelea
na kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo kwa Wilaya ya Magharibi
“A”Mkoa wa Mjini Magharibi.[Picha na Ikulu] 16/07/2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...