Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia) na mkewe Bi. Neema Mwigulu Lameck Nchemba, wakihesabiwa na Karani wa Sensa Bi. Rosemary Shani, katika zoezi la Sensa ya watu na Makazi, kijijini kwao Misigiri Kiomboi Iramba Mkoani Singida leo tarehe 23 Agosti, 2023.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (kulia) akiuliza jambo kwa watu waliopo katika makazi yake (hawapo pichani), wakati wa zoezi la Sensa ya watu na Makazi, kijijini kwake Misigiri Kiomboi Iramba Mkoani Singida.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Singida.)

 

Na. Peter Haule, WFM, Singida

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amewataka wananchi wote ambao hawajafikiwa na zoezi la sensa kuendelea kutenga muda na pia wakifikiwa watoe ushirikiano kwa makarani wa sensa kwa kutoa taarifa sahihi

Dkt. Nchemba ameyasema hayo kijijini kwake Misigiri Kiomboi Iramba mkoani Singida baada ya kuhesabiwa wakati wa zoezi la Sensa ya watu na Makazi lililoanza rasmi leo tarehe 23 Agosti 2022, nchini kote.

Alisema kuwa ni vema wananchi wote wakatoa taarifa zikiwemo za makundi maalumu wakiwemo walemavu ili taarifa hizo ziweze kumsaidia Mhe. Rais  katika masuala ya kupanga mipango ya maendeleo na utekelezaji wa bajeti.

Dkt. Nchemba amesema kuwa amefurahia zoezi la Sensa kwa kuwa maswali yote aliyoulizwa hayakuwa na utata bali yalikuwa ya maendeleo.

Alisema kuwa karani amekuja kwa wakati na ametumia utaratibu uliozingatia maandalizi ya sensa ya watu na makazi yaliyofanyika.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...