Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma leo tarehe 23 Agosti, 2022 ameshiriki katika zoezi maalum la Sensa ya Watu na Makazi lililoanza nchini.
Mhe. Prof. Juma ameshiriki zoezi hilo kwa kuhesabiwa na Karani wa Sensa, Bi. Yvonne Ngakongwa alipomtembelea nyumbani kwake Oysterbay barabara ya Kajificheni jijini Dar es Salaam.
Hivi karibuni, Mhe. Jaji Mkuu alisema kuwa, “Kwa upande wa Mahakama, Sensa ni zoezi muhimu sana kwa sababu inatupa idadi sahihi ya watu itakayosaidia kuboresha zaidi huduma za utoaji haki kwa wananchi.”
Mhe. Prof. Juma alisema hivyo, na kutoa rai kwa wananchi kushiriki katika zoezi hilo muhimu kwa uboreshaji wa huduma za utoaji haki na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
MATUKIO KATIKA PICHA JAJI MKUU WA TANZANIA, MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA ALIPOSHIRIKI ZOEZI LA SENSA.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis (kushoto) akihojiwa na Karani wa Sensa, Bi.Yvonne Ngakongwa alipomtembelea nyumbani kwake Oysterbay barabara ya Kajificheni leo tarehe 23 Agosti, 2022 kwa zoezi maalum la Sensa ya Watu na Makazi lililoanza leo nchini.
Mwenza wa Jaji Mkuu, Bi. Marina Juma akishiriki katika zoezi la kuhesabiwa walipotembelewa na Karani wa Sensa, Bi. Yvonne Ngakongwa.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...