Bondia wa Ngumi za kulipwa kutoka Mkoani Morogoro, Karim Mandonga amewataja Mabondia wa kulipwa ambao hatoweza kupigana nao hata angepewa kiasi gani cha fedha, Mandonga amedai Mabondia hao wapo upande wa timu yake.
Mandonga amewataja Mabondia hao ni Twaha Kassim (Kiduku), Selemani Kidunda na Mfaume Mfaume, amesema hapa nchini anaweza kupigana na Bondia yoyote atakayejitokeza.
“Bondia hupaswi kuchagua mtu wa kupigana naye, hiyo ni kazi ya Promota wa pambano, Bondia ukipewa Mpinzani yeyote unapaswa kupigana naye”, amesema Mandonga.
“Mabondia wa nje ya nchi, siwezi kupigana nao ni Mike Tyson na Floyd Mayweather, lakini wengine wote nacheza nao”, ameeleza.
Bondia wa Ngumi za kulipwa kutoka Mkoani Morogoro Karim Mandonga akimchakaza mpinzani wake Omary Musa na kuibuka na ushindi wa Ko raundi ya kwanza ikiwa sehemu ya sherehe za kuhamasisha zoezi la sensa ya watu na Makazi iliyofanyika katika viwanja vya leaders club jijini Dar es salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...