

Na John Walter-Babati
Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Daniel Sillo ametoa mabati 600 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa miradi ya elimu na afya jimboni humo.
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo agosti 26,2022 katika ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Babati ikiwa ni mkakati wa Mbunge huyo (CCM) kusaidia kukamilisha miradi ya afya na elimu inayoendelea kujengwa wilayani hapo.
Mbunge huyo ametoa mabati hayo kwa mgawanyo katika vijiji sita vya Tsamas (150), ,Secheda (117),Boay (84),Kisangaji (29),Datar (110) na Yorotonik (110).
Amewataka madiwani na watendaji wengine kusimamia bati hizo zikatumike kwenye miradi iliyokusudiwa.
Aidha ameishukuru benki ya NMB kwa msaada huo walioutoa ambao umetokana na mahusiano mazuri waliyonayo yeye na benki hiyo.
Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Babati imempongeza Mbunge Sillo kwa jitihada za kuwaletea wananchi maendeleo kama inavyoelekeza ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza kwa niaba ya madiwani, diwani wa kata ya Ufana Bernad Bajuta amesema mabati hayo yatasaidia sana kumaliza miradi ya elimu na afya iliyokwama kwa muda mrefu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...