Kulingana na kuongezeka kwa mikakati ya maendeleo ya sekta ya nishati nchini Tanzania, CEO Roundtable - Tanzania (CEOrt) imewakutanisha viongozi wafanyabiashara kwa ajili ya majadiliano kuhusu “Kuendesha Ushiriki wa Sekta Binafsi kwenye Sekta ya Nishati”. Taarifa za hivi karibuni katika sekta ya nishati nchini ni pamoja na mipango kuhusu bomba la EACOP, maendeleo ya mitambo ya gesi ng’ambo, makubaliano katika mradi wa gesi asilia iliyosindikwa (LNG) na mapendekezo kadhaa ya mradi wa nishati mbadala. 

Katika wakati ambapo mabadiliko ndani ya sekta ya nishati yanaendelea duniani, washikadau wanatilia maanani matokeo yake kwa fursa zinazoibuka barani na pia maamuzi ya uwekezaji yanayopaswa kufanywa. Awamu inayofuata katika sekta ya nishati nchini Tanzania inatarajiwa kujikita katika kukuza uwekezaji na ukuaji, hivyo basi kuwafanya viongozi wa sekta binafsi kuwa kipengele muhimu kwa kutegemea michango yao ya kimkakati na ushiriki wao katika kufungua fursa chipukizi nchini.

CEOrt ilimkaribisha Mhe. January Makamba, Waziri wa Nishati wa Tanzania, akiwa Mgeni Rasmi katika hafla hiyo. Mhe. Makamba amesisitiza azma ya Serikali ya kuweka uwiano wa maendeleo ya nishati vijijini na mijini, na kutaja vipaumbele kuwa ni pamoja na kuboresha ufanisi wa nishati sambamba na kuongeza utegemezi wa sekta hiyo, na kuhimiza ushiriki wa sekta binafsi ya ndani katika mnyororo wa thamani wa nishati mbalimbali nchini.

Madhumuni mengine muhimu ya sekta hii ni kupunguza ukataji miti, lengo ambalo CEOrt inakusudia kusaidia kulifanikisha kwa vile linaendana na msimamo wa jukwaa hilo wa kuchukua hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Ikiwa imedhamiria kuboresha ushirikiano na Serikali, CEOrt inatazamia kuwezesha mazungumzo haya kati ya Waziri wa Nishati na viongozi wa sekta binafsi ili kuchunguza zaidi jukumu la Nishati katika kuleta maendeleo endelevu na mafanikio ya nchi.

CEO Roundtable - Tanzania ni Shirika linawakilisha Wakurugenzi Wakuu kutoka kampuni zaidi ya 160 zinazoongoza nchini Tanzania kutoka sekta mbalimbali za uchumi kwa madhumuni ya pamoja ya kuongeza matokeo katika uongozi na ustawi endelevu wa jamii na uchumi wa nchi. Kwa pamoja, wanachama wa CEOrt huchangia katika uchumi wa Tanzania kupitia ukusanyaji wa kodi, ajira, kujenga uwezo, kuhamisha teknolojia na kuongeza ujuzi.

Mhe. January Makamba, Waziri wa Nishati

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...