Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan mapema leo ameshiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linalofanyika Nchi nzima.
Akizungumza na Karani wa Sensa Bi. Phausta Ntigiti wakati alipokuwa akihesabiwa katika Makazi yake Chamwino, Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 23 Agosti, 2022 kwenye shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi pia amezungumza na na vyombo vya habari kuhamasisha ushiriki wa Wananchi huku akibainisha dodoso muhimu za kujaza pindi karani wa Sensa anapofika eneo la mkazi kwa ajili ya zoezi la kuhesabu kaya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Karani wa Sensa Phausta Ntigiti wakati alipokuwa akihesabiwa katika Makazi yake Chamwino Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 23 Agosti, 2022 kwenye shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuhesabiwa katika Makazi yake Chamwino Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 23 Agosti, 2022 katika shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...