Na Vero Ignatus Arusha


Sekta ya AFYA imetajwa kuwa ni sekta nyeti kwani inayo kazi kuwaandaa wataalam vizuri ili kuboresha utoaji wa huduma za Afya ikiwemo kushughukika na mwili wa binadamu,na kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa na Afya bora ,siyo kazi rahisi inahitaji umakini mkubwa

Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa John Mongela katika hafla ya uzinduzi wa Chuo cha Kilimanjaro Institute of Health Sciences Arusha, na kusema kuwa sekta hiyo haiwezi kufanywa na mtu ambaye siyo mtaalam na mbobezi ,kwani mahitaji ya watumishi wenye weledi kwenye Sekta ya Afya ni mkubwa

"Chuo hiki ni kwasababu ya mafunzo ya sekta ya Afya, kama mnavyojua serikali yetu ya awamu ya sita chini ya Mhe.Rais Samia Sukuhu Hassan, kuna kazi kubwa sana inafanywa katika kuboresha huduma za jamii, ikiwemo shule, barabara, miradi ya maji umeme na maeneo mengine, ikiwemo zahanati kwenye vijiji, vituo vya Afya kwenye tarafa, hospital za wilaya zinajengwa"alisema Mongela

Mongela amesema Uongozi, wadau na wawekezaji katika kufungua chuo hicho pamoja na Kanisa la Baptist, wanaatembea maono ya serikali ya awamu ya sita, kwani serikali peke yake haina namna ya kufanya vitu vyote, balii inategemea juhudi za wawekezaji binafsi, sekta binafsi, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kwaajili ya kuleta maendeleo

Ametoa Rai kwa vile ni sekta ya AFYA na Sayansi amewataka kuzingatia sheria kanuni kwasababu mmesajikiwa na Mamlaka zinazo husika za kiserikali, wafuate miongozo ili watakaokuja kutoa mafunzo ,watoke wakiwa na uweledi wa kutosha na waweze kuchangi kuimarisha Afya za Watanzania pamoja na kuchangia maendeleo ya kasi ya nchi

"Mimi niwapongeze sana kanisa la Baptist kwa kuruhusu eneo hili litumike kwa faida kwa jamiina nchi yetu, na mkoa wetu"alisema Mongela

Nae Mkurugenzi wa chuo hicho Dkt Shabani Amir Mwanga,amesema Taasisi hiyo imesajiliwa na Baraza la elimu Nacte, na kutambuliwa na Wizara ya Afya na Mabaraza yote ya wataalam, hivyo kinatoa kozi za Afya,ambapo hadi sasa wamesajili wanafunzi 300 kujiunga na mafunzo katika levo ya diploma kwa maana ya (Diploma in clinicle Medicine) na (Diploma in Pharmaceutical science)

"Kwa kuanzia 9 Septemba 2022 wanafunzi wataanza kuripoti katika chuo hicho ambapo hadi hivi sasa wanafunzi ambao wameshasajiliwa kuanza masomo rasmi ni 9octoba 2022 ni wanafunzi takribani 300,na tumetoa ofa kwa wanafunzi 10 wa jamii ya inayotuzunguka kusoma bure watakaookamilisha mchakato wa kujisajili"alisema Mwanga

Dkt Mwanga amesema kuwa mwaka huu 2022 wataanza na kozi mbili ,ikiwemo pharmacy na Clinical Medicines, ambapo matarajio hadi mwakani 2023, ni kuhakikisha Taasisi hiyo ya Kilimanjaro Institute of Health science Arusha, inakuwa na programu za Digrii, kwani wameshaingia mikataba (MOU) na Hospitali kuu za Arusha kwamba ziwe ndiyo Hospitali kuu za kufundishia

Kwa upande wake Askofu wa kanisa la Baptist Tanzania Anord Manase: "Kutekeza siyo kuanguka" Chuo cha Kanisa sasa tunarudi kwa upya tukiwa na malengo mapya kabisa kwaajili ya maendeleo ya Taifa na Jamii kwa ujumla katika kutoa Elimu na Afya.

Askofu Manase amesema wameingia kwenye makubaliano kwaajili ya kutoa Elimu ya Afya,ambapo amesema kwa upande wao kama kanisani wapo tayari kutoa ushirikiano kwa serikali na
Mahali wanapowahitaji kama kanisa kushiriki katika shughuli za maendeleo ya ya Taifa tayari.

Wameahidi kuzifuata taratibu zote pamoja na kufanya kazi kwa bidiii ili kuhakikisha chuo hicho kinaketa mabadiliko sahihi kwaajili ya kutoa walaalam wakwenda kuisaidia jamii ya Watanzania.

Aidha chuo hicho cha Kilimanjaro Institute of Health science Arusha kipo nchi nzima ambapo wana Tawi Mwanza, Dodoma, Dar es salaam na Arusha,hivyo kwa Wanafunzi wote watakaoingia chuoni hapo mwaka huu 2022 watapata chakula cha mchana bure kama na Hosteli bure kama ofa ya chuo



Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela Kilimanjaro Institute of Health Sciences Arusha akipongezana na mkuu wa chuo cha Shabani Amir Mwanga mara baada ya uzinduzi rasmi wa chuo hicho kilichopo Ngaramtoni
Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela wakizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Chuo cha Kilimanjaro Institute of Health science Arusha
Mkurugenzi wa Chuo cha Kilimanjaro Institute of Health science Arusha Dkt.Shabani Amir Mwanga akizungumza katika hafla ya uzinduzi wabchuo hicho kilichopo Ngaramtoni

Kutoka kushoto ni Askofu Mkuu Kanisa la Wabaptist Tanzania Arnold Manase akimkabidhi kupaza sauti mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela kuzungumza na wageni waalikwa pamoja na waafanyakazi wa chuo hicho
Wa pili kutoka kushoto ni Askofu Mkuu Kanisa la Wabaptist Tanzania Arnold Manase,kushoto kwake ni mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akifuatiwa na Mkurugenzi wa Chuo cha Kilimanjaro Institute of Health science Arusha Dkt. Shabani Amir Mwanga pamoja na baadhi ya viongozi wengine
Baadhiiya wageni waalikwa wakiendelea kufuatilia kile kinachoendelea katika uzunduzi wa Chuo cha Kilimanjaro Institute of Health science Arusha
Baadhi ya wafanyakazi wa chuo cha Kilimanjaro Institute of Health science Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi

Baadhi ya wageni waalikwa wakiendelea kufuatilia kile kinachoendelea katika uzunduzi wa chuo cha Kilimanjaro Institute of Health science Arusha

Baaadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja na mmgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Chuo cha Kilimanjaro Institute of Health science Arusha




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...