
MWENYEKITI wa kampuni ya TOL Gases Ltd inayozalisha ges ya Hospitalini ‘Oksejeni’ na gesi ya viwandani ‘Gesi Mkaa’ Michael Shirima akizungumza na wanahisa katika mkutano mkuu wa wanahisa wa Tol Gases Ltd , uliofanyika jana katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kwaajili ya kujadili mafanikio ya kampuni hiyo. Kuanzia kushoto ni Prof; Abraham Temu, Eng; Joseph Machenge, Adv. Collineries Kiliwa , Mwenyekiti Michael Shirima, mkurugenzi Daniel Warungu, mkurugenzi Simon Mponji
Kampuni imeweza kukuza kiasi cha gawio ukilinganisha na gawio la shilingi 34.78 kwa hisa kwa mwaka 2020. Taarifa za fedha za kampuni kwa mwaka unaoishia Desemba 2021 zinaonyesha kukua kwa mapato kwa asilimia 25, kutoka shilingi bilioni 19.8 kwa mwaka 2020 hadi shilingi bilioni 24.8, ambapo faida baada ya kodi ilikua kwa asilimia 41 kutoka bilioni 2.3 kwa mwaka 2020 hadi bilioni 3.3 kwa mwaka 2021.
Ukuaji wa mapato ya kampuni hiyo umechangiwa na maboresho ya kiutendaji yaliyofanyika hivi karibuni sambamba na mikakati ya upanuzi iliyochangia kuimarisha nafasi ya kampuni kama mzalishaji na muuzaji wa gesi za viwandani na hospitalini pamoja na kupanua wigo wake wa usambazaji bidhaa katika nchi nyingine za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kama vile Zambia, Zimbabwe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Malawi.
Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi wa kampuni ya TOL Gases, Michael Shirima, alipongeza maboresho ya kiutendaji na jitihada zilizofanywa na kampuni katika kuhakikisha upatikanaji wa hewa ya Oksijeni inayotumika mahospitalini wakati wa mlipuko wa Uviko-19.
"Kutokana na ugonjwa wa Uviko-19, mwaka 2021 ulikuwa na changamoto nyingi katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa ujumla. Nina furaha kuripoti kwamba tulifanikisha lengo letu la kuisaidia serikali kuhakikisha upatikanaji wa gesi ya Oksijeni katika kipindi kile kigumu, na ninaipongeza Kampuni kwa kuhakikisha upatikanaji wa gesi hiyo muhimu katika vituo mbalimbali vya huduma za afya."
Mbali na kuripoti ongezeko la faida kwa mwaka 2021, TOL Gases Limited imeelezea mikakati mbalimbali inayotarajiwa kukuza matokeo ya kifedha ya Kampuni. Hivi karibuni Kampuni imezindua mradi wa mpya ambao ni wa pili katika Wilaya ya Rungwe na utakuza uwezo wa Kampuni wa kuzalisha gesi ya ukaa.
Akizungumzia mradi mpya wa gesi ya ukaa, Mwenyekiti alisema, "Kiwanda hiki kipya kitaongeza uwezo wa Kampuni wa kuzalisha gesi ya ukaa na kinatarajiwa kukuza mapato ya kampuni kwa kiasi kikubwa. Aidha, kampuni imewekeza katika magari mapya ya usambazaji ili kuimarisha nafasi yake kama mzalishaji na msambazaji wa kuaminika wa gesi za viwandani na hospitalini."
Mradi mpya wa gesi ya ukaa upo katika kijiji cha Ikama, Wilayani Rungwe jijini Mbeya na unatarajiwa kukuza mapato ya kila mwezi kwa takribani shilingi bilioni 8.2, ikiwa ni ongezeko la asilimia 42 la mapato yatokanayo na uzalishaji wa gesi ya ukaa pekee.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...