Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Benki ya NMB Plc wamesaini Hati ya Makubaliano ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub).
Makubaliano hayo yamesainiwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora Balozi James Bwana kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine na Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Bw. Alfred Shao kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Akiongea katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo Balozi Bwana amesema mfumo huo wa kidigitali utaisaidia Serikali kuwatambua, kuwasajili na kuwawezesha Diaspora wa Tanzania waliopo sehemu mbalimbali ulimwenguni kupata huduma mbalimbali na kushiriki kidigitali katika shughuli mbalimbali za maendeleo, biashara, uchumi na uwekezaji nchini.
“Ushirikiano wa Wizara na Benki ya NMB Plc ni wa muda mrefu na wenye mafanikio mengi katika kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo ya Tanzania. Wizara ina imani kuwa kupitia udhamini huu wa shilingi milioni 100 kutoka Benki ya NMB, fedha hizo zitawezesha kukamilisha matengenezo ya mfumo wa Diaspora Digital Hub na hivyo kuboresha huduma zenye kukidhi mahitaji ya Diaspora wote ulimwenguni,” amesema Balozi Bwana
Balozi Bwana ameongeza kuwa, mfumo huo pamoja na mambo mengine, utafungua uwezekano wa fursa zaidi za ushirikiano kati ya Wizara na Benki hiyo utawezesha utunzaji wa taarifa mbalimbali za Diaspora wa Tanzania popote walipo ulimwenguni na hivyo kurahisisha kazi ya uratibu wa Diaspora.
Balozi Bwana amesema Serikali inategemea kuwa kukamilika kwa mfumo huo kutaweza kuwatambua, kuwasajili na kuwawezesha Diaspora wa Tanzania Duniani kote kupata huduma nyingi na muhimu wanazohitaji na kushiriki kidijitali katika shughuli mbalimbali za maendeleo biashara, uchumi na uwekezaji hapa nchini.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bw. Alfred Shao amesema benki yao inaamini kuwa kukamilika kwa mfumo huo kutawawezesha Diaspora wa Tanzania kuungana, kutambulika na kuiwezesha Serikali kuwa na Kanzi Data ya uhakika na kuwafikia diaspora wengi kwa wakati mmoja na hivyo kuleta mafanikio makubwa kwa Taifa na Mtanzania mmoja mmoja anayeishi nje ya nchi.
"Sisi NMB tunaamini kuwa mfumo huu, utawaunganisha, utawatambua na kuiwezesha Serikali kuwa na Kanzidata ya Diaspora wake, ni wazi kuwa mfumo huu utaleta maendeleo makubwa kwa Taifa na Mtanzania mmoja mmoja wanaoishi nje ya nchi," alisema Bw. Shao
Aliahidi kuwa NMB itaendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika kuhakikisha mfumo wa kidigitali wa Diaspora Digital Hub unakamilika kwa wakati.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Semeni Nandonde amesema makubaliano yaliyoingiwa kati ya Wizara na Benki ya NMB yanaashiria utayari wao katika kulifadhili na kuliwezesha wazo la Wizara la kuwa na mfumo wa kutunza taarifa za Diaspora na kuwawezesha dispora kunufaika na huduma mbalimbali pindi mfumo huo utakapokamilika.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana akizungumza katika hafla ya utiaji saini hati za makubaliano ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) kati ya Wizara na Benki ya NMB PLC katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Semeni Nandonde (aliyesimama
kukulia) akizungumza wakati wa hafla ya kusaini hati za makubaliano ya
kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za
Diaspora, (Diaspora Digital Hub) kati ya Wizara na Benki ya NMB katika
Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam .
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi James Bwana (kulia) na Mwakalishi wa Mtendaji Mkuu wa
Benki ya NMB, Bw. Alfred Shao (kushoto) wakisaini hati za makubaliano ya
kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za
Diaspora, (Diaspora Digital Hub) walizosaini katika Ofisi ndogo za
Wizara jijini Dar es salaam .
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi James Bwana (kulia) na Mwakalishi wa Mtendaji Mkuu wa
Benki ya NMB, Bw. Alfred Shao (kushoto) wakionesha hati za makubaliano
walizosaini ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza
taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) walizosaini katika Ofisi
ndogo za Wizara jijini Dar es salaam .
Mwakilishi
wa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bw. Alfred Shao akizungumza katika
hafla ya kusaini Hati ya Makubaliano ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data
wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) na
Benki ya NMB PLC.
Watumishi
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika
picha ya pamoja baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya kutengeneza
Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora,
(Diaspora Digital Hub) na Benki ya NMB PLC.
Watumishi
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na
Watumishi wa Benki ya NMB Plc katika picha ya pamoja baada ya kusaini
Hati ya Makubaliano ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa
kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...