Na. Damian Kunambi, Njombe.

Mwenyekiti wa zoezi la sensa ya watu na makazi wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Andrea Tsere amesema ameridhishwa na mwenendo wa zoezi hilo ambapo ndani ya siku mbili wameweza kufikia asilimia zaidi ya 50 huku tarafa ya Masasi ikitajwa kufanya vizuri zaidi.

Hayo ameyasema alipokuwa katika ziara ya kukagua zoezi hilo na kuongeza kuwa watu wamekuwa na mwitikio mzuri huku changamoto zilizojitokeza zikiwa chache ikiwemo mmoja wa wazee aliyefahamika kwa jina la Stella Haule mkazi wa kata ya Nkomang'ombe kukataa kuhesabiwa kwa madai ya kuondolewa katika kundi la wanufaika wa kaya masikini (TASAF).

Hata hivyo imeelezwa kuwa mzee huyo alipewa elimu na kisha akakubali kuhesabiwa hivyo mpaka sasa zoezi hilo linaendelea vyema.

Sanjali na hilo pia mkuu huyo amewataka makalani wote na wasimamizi kuendelea kutoa elimu kwa watu ambao wataonekana kutokuwa na utayari wa kuhesabiwa kwani huenda wanakataa kwa kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya zoezi hilo .





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...