Na.Khadija Seif, Michuzi Tv .


KUELEKEA pambano la Kitaifa kati ya Twaha Kiduku na Bondia kutoka Misri Abdo Khaled  wanamichezo hususani mchezo wa Masumbwi wametakiwa kuvunja matabaka na kuungana Kwa pamoja na kumtakia heri bondia Twaha Kiduku kufanya vizuri septemba 24 katika viwanja vya Nangwanda sijaona Mkoani Mtwara kwa maslahi ya Taifa la Tanzania.

Akizungumza Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa amesema makando kando hayana Msingi pale Taifa linapomteua mtu akatuwakilishe kitaifa katika Michezo badala yake nguvu na hamasa zitumike kumpa moyo wa kufanya vizuri mchezaji huyo.

Hata hivyo ameeleza kuwa Wizara yake  itampa ushirikiano wa kutosha na inamuunga Mkono Bondia huyo ili kuleta chachu ya ushindi wake ambao Taifa litajuvunia kutokana na ubingwa wake katika mchezo wa Masumbwi nchini.

Aidha amemtaja Kiduku ambae ana wania mkanda wa UBO ni Miongoni mwa Mabondia wanaofanya vizuri ambao kimsingi anatambua nafasi yake katika kuweka Ramani ya Mchezo wa Masumbwi  Kitaifa na Kimataifa.

"Anapokuwa ulingoni anafanya vizuri na unamuona ana kiu yakuhitaji ushindi hivyo wizara kwa pamoja tunamuunga mkono na kumtakia ushindi dhidi ya mpinzani wake kutoka Misri kwani ushindi wake ni wataifa kwa ujumla sio wake peke yake."

Pia ametoa wito kwa viongozi wa halmashauri,wakurugenzi na wakuu wa wilaya kuwaeka pamoja na kuwapa hamasa wananchi wao kushiriki katika Michezo mbalimbali ili kuimarisha miili yao.

"Tunaibeba kauli mbiu ya pambano hili "Ubabe ubabe tu" iende katika kila wilaya,mikoa na kila mitaa ikaamshe vipaji vingine katika Michezo na pia viongozi kwa ujumla wahakikishe wanaleta hamasa kwa wananchi wao kuhakikisha Michezo inapewa nafasi kubwa kwenye jamii."



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...