Na Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI imesema inathamini suala la usalama wa chakula kwani ndio mhimili mkubwa wa afya ya watanzania na ukuaji wa uchumi.
Hayo yameelezwa leo Septemba 20 Jijini Dodoma na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma,Dk Fatma Mganga wakati akifungua mafunzo kwa watumishi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Dk Mganga amesema Serikali ya awamu ya sita inathamini suala la usalama wa chakula kwani ndio mhimili mkubwa wa Afya ya watanzania na ukuaji wa uchumi.
" Nimetonywa kwamba, kupitia mafunzo haya mtajengewa uwezo kuhusu sheria na Kanuni ya Viwango, Mwongozo wa Utekelezaji wa Majukumu ya ushirikiano baina ya TBS na Halmashauri, ukaguzi, uchukuaji sampuli na uteketezaji na utaratibu wa usombaji na usajili wa maeneo yanayotumika kuuza vyakula.
"Ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya yataongeza umahiri wetu katika kusimamia usalama wa chakula na hivyo mtaweka mikakati madhubuti ya kusimamia maeneo yenu na kuhakikisha hakuna changamoto yoyote,"amesema Dk.Mganga.
Aidha, Sheria ya Afya ya Jamii ya mwaka 2009 na kanuni zake, sheria ya usimamizi wa usalama wa chakula na kanuni zake, pamoja na sheria ndogo za halmashauri zenu zitumike vizuri kuhakikisha maeneo yetu yanakuwa salama.
"Nichukue fursa hii kutoa pongezi nyingi kwa Serikali kukasimu baadhi ya majukumu kwa Wataalam wetu wa Halmashauri ambao wapo karibu zaidi na wadau,"amesema Katibu Tawala huyo.
Amesema kupanuliwa kwa wigo huo kutasaidia sana kufichuo vitendo viovu vilivyokuwa vinafanywa na watu wenye tamaa ya kujitajirisha kwa kuuza bidhaa ambazo hazikidhi viwango vinavyotakiwa au bidhaa zenye viambata sumu.
Amesema sheria hiyo sasa inaenda kuwaongezea nguvu ya usimamizi wakishirikiana na TBS na hivyo kupunguza au kuondoa changamoto zilizopo sasa.
"Niwaase mkatekeleze majukumu hayo kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu ambazo zitafafanuliwa katika mafunzo haya.
"Sitavumilia mtaalam ambaye atafanya kinyume na kutumia mamlaka mnayokasimiwa kusumbua wazalishaji ambao wanajitahidi kuzingatia miogozo iliyopo.
"Tutumie muda wetu mwingi kuelimisha zaidi kabla ya kuchukua hatua za kuadhibu,"amesema Dk.Mganga
Aidha, amewataka kuhakikisha wakirudi katika vituo vyao vya kazi wanatumia mafunzo hayo vizuri.
"Hii ndio njia muafaka itakayowezesha kuhakikisha watumiaji wanapata bidhaa salama,"amesema Katibu Tawala huyo.
Kwa upande wake Meneja wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kati,Nickonia Mwabuka amesema lengo Kuu la mafunzo hayo ni kuwapa walengwa kujua sheria,kanuni na taratibu zinazohusu utekelezaji wa majukumu baina ya Tamisemi na TBS.
Amesema mafunzo hayo yamewalenga watumishi wa idara ya afya na biashara katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
"TBS imeekuwa ikifanya shughuli za ukaguzi na udhibiti kwa kushirikiana na watumishi kutoka katika Ofisi za Halmashauri hivyo naamini mafunzo haya yataleta ufanisi katika maeneo yao ya kazi,"amesema
Bw.Mwbuka amesema TBS inatambua mchango wa wafanyakazi katika Ofisi mbalimbali hivyo itaendelea kutoa mafunzo kwa watumishi hao.
KATIBU
Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dk.Fatma Mganga,akizungumza wakati wa ufunguzi
wa Mafunzo kwa Watumishi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
yaliyowalenga Watumishi kutoka Idara ya Afya na Idara ya Biashara Ofisi
ya Rais Tamisemi na kuhudhuriwa na Maafisa biashara kutoka Mkoa wa
Dodoma na Halmshauri zote yaliyoandaliwa na TBS yaliyofanyika leo
Septemba 20,2022 jijini Dodoma.
KATIBU
Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dk.Fatma Mganga,akisisitiza jambo kwa
washiriki (hawapo pichani) wakati wa Mafunzo yaliyowalenga Watumishi
kutoka Idara ya Afya na Idara ya Biashara Ofisi ya Rais Tamisemi na
kuhudhuriwa na Maafisa biashara kutoka Mkoa wa Dodoma na Halmshauri zote
yaliyoandaliwa na TBS yaliyofanyika leo Septemba 20,2022 jijini Dodoma.
SEHEMU
ya washiriki wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dk.Fatma
Mganga,(hayupo pichani) wakati wa Mafunzo yaliyowalenga Watumishi kutoka
Idara ya Afya na Idara ya Biashara Ofisi ya Rais Tamisemi na
kuhudhuriwa na Maafisa biashara kutoka Mkoa wa Dodoma na Halmshauri zote
yaliyoandaliwa na TBS yaliyofanyika leo Septemba 20,2022 jijini Dodoma.
KATIBU
Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dodoma Bi.Aziza
Mumba,akizungumza wakati wa Mafunzo kwa Watumishi wa Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa yaliyowalenga Watumishi kutoka Idara ya Afya na Idara
ya Biashara Ofisi ya Rais Tamisemi na kuhudhuriwa na Maafisa biashara
kutoka Mkoa wa Dodoma na Halmshauri zote yaliyoandaliwa na TBS
yaliyofanyika leo Septemba 20,2022 jijini Dodoma.
MENEJA
wa Kanda ya Kati wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.Nickonia
Mwabuka,akitoa taarifa ya ufunguzi wa Mafunzo kwa Watumishi wa Tawala za
Mikoa na Serikali kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt.Athuman
Ngenya yaliyofanyika leo Septemba 20,2022 jijini Dodoma.
Mratibu
Huduma za Afya na Usafi TAMISEMI Selemani Yondu,akitoa neno la shukrani
kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dk.Fatma Mganga,mara baada ya
kufungua Mafunzo kwa Watumishi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
yaliyowalenga Watumishi kutoka Idara ya Afya na Idara ya Biashara Ofisi
ya Rais Tamisemi na kuhudhuriwa na Maafisa biashara kutoka Mkoa wa
Dodoma na Halmshauri zote yaliyoandaliwa na TBS yaliyofanyika leo
Septemba 20,2022 jijini Dodoma.
KATIBU
Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dk.Fatma Mganga,akiwa katika picha ya pamoja
mara baada ya kufungua Mafunzo kwa Watumishi wa Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa yaliyowalenga Watumishi kutoka Idara ya Afya na Idara
ya Biashara Ofisi ya Rais Tamisemi na kuhudhuriwa na Maafisa biashara
kutoka Mkoa wa Dodoma na Halmshauri zote yaliyofanyika yaliyoandaliwa na
TBS leo Septemba 20,2022 jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...